KOREA KASKAZINI HAIJIBU MAWASILIANO YA MAREKANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 15 March 2021

KOREA KASKAZINI HAIJIBU MAWASILIANO YA MAREKANI

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jonh-un.

UTAWALA wa Rais Joe Biden wa Marekani umesema umekuwa ukijaribu kuwasiliana na serikali ya Korea Kaskazini tangu mwezi Februari lakini bado haijapata jibu. Marekani imejaribu kuwasiliana na Korea Kaskazini kwa namna mbalimbali kuzuia wasiwasi unaoendelea kujitokeza, maafisa wamesema.

Marekani na Korea Kaskazini bado zina hitilafiana juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na ule wa utengenezaji makombora. Mikutano mitatu kati ya mtangulizi wa Bwana Biden na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jonh-un ilifikia machache tu.

Mazungumzo yalishindwa kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia - hitaji la msingi kwa Marekani na nchi zingine za Magharibi zenye nguvu. Vyombo vya habari vya Korea kaskazini bado havijamkubali Joe Biden kama rais wa Marekani.

Majaribio ya Marekani kuwasiliana na Pyongyang yamejumuisha "New York Channel" - kupitia ujumbe wa Korea Kaskazini wa Umoja wa Mataifa.

Afisa wa Marekani amezungumza na Shirika la Habari la Reuters na kuliarifu kwamba nchi hiyo "imejaribu mara kadhaa" kuwasiliana na Korea Kaskazini kwa zaidi ya miezi 12 bila mafanikio yoyote, ikiwa ni pamoja na mwaka wa mwisho wa Donald Trump kama rais.

Bwana Biden tayari ametangaza kupitiwa tena kwa sera za Korea Kaskazini ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa Aprili.

Amemuita Bwana Kim kuwa jambazi na kusisitiza haja ya Korea Kaskazini kuachana kabisa na mpango wake wa nyuklia kabla ya Marekani na Umoja wa Mataifa kuindolea nchini hiyo kikwazo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameendelea kusisitizia uwezo wa nchi yake kijeshi, na kuendelezaji utengenezaji wa mabomu ya masafa marefu, vichwa vya makombora, setilaiti za ujasusi na nyambizi za nyuklia. Wakati huohuo, ametoa wito kwa Marekani kuachana na "sera zake za kichokozi".

Malengo ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yanatarajiwa kujitokeza zaidi wiki hii wakati wa ziara nchini Japani na Korea Kusini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken and Defence Secretary Lloyd Austin.

Uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini ulizorota mwaka 2017 wakati ambapo Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kupiga maeneo ya Marekani.

Wasiwasi ulipungua kidogo wakati Bwana Trump alipoahidi kuimarisha uhusiano wa kibinafsi na Bwana Kim.

-BBC

No comments:

Post a Comment