JESHI LA POLISI LATOA HUDUMA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA PUGU-MNADANI, DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 17 March 2021

JESHI LA POLISI LATOA HUDUMA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA PUGU-MNADANI, DAR

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Kata ya Pugu Mnadani waliofika kupata huduma anuai za 'One Stop Center' (OSC) eneo hilo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Kata ya Pugu Mnadani waliofika kupata huduma anuai za 'One Stop Center' (OSC) eneo hilo.


Mratibu wa OSC katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mkaguzi Msaidizi, Dk.  Christina Onyango (kulia) akitoa elimu juu ya huduma zinazotembea za mkono kwa mkono maarufu ‘One Stop Center (OSC) kwa wananchi kabla ya kupatiwa huduma anuai eneo hilo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi akiwasikiliza baadhi ya wananchi wa eneo la Kata ya Pugu Mnadani waliofika kupata huduma.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi akiwasikiliza baadhi ya wananchi wa eneo la Kata ya Pugu Mnadani waliofika kupata huduma.

Mratibu wa OSC katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mkaguzi Msaidizi, Dk.  Christina Onyango (wa pili kulia) akitoa taarifa fupi juu ya mwenendo wa huduma hizo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi akizungumza na baadhi ya wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua huduma hiyo eneo la Kata ya Pugu Mnadani.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala linaendesha huduma zinazotembea za mkono kwa mkono maarufu ‘One Stop Center (OSC) kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kubaini vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata ya Pugu Mnadani na kuwahudumia.

Akizungumza alipozindua huduma hizo eneo la Pugumnadani, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, ACP Janeth Magomi amesema huduma hizo ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoiadhimishwa kitaifa na kimataifa, Machi, 8. Kamanda Magomi alisema huduma hizo zinazoambatana na msaada wa kisheria, huduma za afya na huduma za dawati la jinsia zitatolewa kuanzia Machi 15, 2021 hadi Aprili 1, 2021.

“Ingawa ni maadhimisho ya kumtambua nafasi ya mwanamke katika maendeleo na ustawi wa jamii, hatuwaachi nyuma wala kuwabagua wanaume, bali tunahakikisha wote kuanzia watoto, wanawake na wanaume wana amani na hakuna anayefanyiwa unyanyasaji wala ukatili wa kijinsia,” alisema Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi alibainisha kuwa huduma hizo zimeanzia eneo la Pugu-Mnadani kwa kuwa lina wakazi wengi kutoka maeneo tofauti na pia, kuna ukatili wa kijinsia wa aina tofautitofauti kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo, alisema ili kuchochea maendeleo ya familia na jamii kwa jumla, wanawake hawapaswi kubweteka na kusubiri kipato pekee kutoka kwa wanaume kwa matumizi ya familia, bali nao kushiriki shughuli halali za uzalishaji mali zikiwamo za ujasiriamali. 

“Wanawake tusibweteke na kusibiri kila kitu kutoka kwa baba; fanya hili na lile kumsaidia; lima au uuza nyanya, mchicha na shughuli nyingine; hii inasaidia familia…” alisema Magomi.

Akifafanua zaidi, Mratibu wa OSC katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mkaguzi Msaidizi, Dk.  Christina Onyango aliyataja maeneo mengine yatakayonufaika na huduma hizo awamu hii ni pamoja na Mazizini- Mombasa katika Kata ya Ukonga, Karakata (Kipawa), Kwa Wagumu (Tabata), Soko la Muslimu (Kata ya Liwiti), Matumbi (Tabata) maeneo ya Michikichini na Pangani (Kata ya Ilala) na eneo la Kombo (Vingunguti).

Dk Onyango alisema taarifa toka kwa baadhi ya wananchi zilibainisha hata wanaume wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili eneo hilo, lakini wamekuwa na soni kujitokeza na kutoa taarifa kwa vyombo husika. Pamoja na hayo alikosoa tabia ya baadhi ya wanajamii kumaliza kienyeji mashauri yanayohusu ukatili na unyanyasaji wa kijinsia , hadi kutnapotokea tofauti katika makubaliano hayo.

“Wengi mnaleta kesi baada ya kukaa na kukubaliana kumalizana kwa kulipa na Yule anayelipa akianza kusumbua kulipa kilichobaki, ndipo mnaleta polisi; hivyo mnakuwa hamumtedi haki mwathirika,” alisema Onyango.

Akitoa elimu mintarafu ushahidi dhidi ya , Dk Onyango alisema anayefanyiwa ukatili huo awahishwe hospitali kabla ya kufanyiwa usafi ili kutopoteza ushahidi.

“Mtoto au binti akifanyiwa ukatili wa kingono labda amebakwa, msiwaoshe wala kuwasafisha, bali muwawahishe hospitali ili msipoteze ushahidi ambao ungemtia hatiani mtuhumiwa; aoshwe baada ya ushahidi kuchukuliwa,” alisema.

Mratibu huyo, alitaja faida nyingine za kumwahisha mwathirika wa ubakaji kuwa ni pamoja na kuwezesha kupewa dawa za kuepusha mimba na kuzuia maambukizi ya ukimwi ndani ya saa 72.


Huduma zikiendelea kwa wakazi wa Kata ya Pugu Mnadani.


Huduma zikiendelea kwa wakazi wa Kata ya Pugu Mnadani.


Wananchi wakisubiri kupata huduma hizo.

No comments:

Post a Comment