Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini,Aidan Komba Akifanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigopesa kwa wakulima wa kilimo cha chai Rungwe mapema wiki iliyopita mkoani Mbeya. |
Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima wa chai wilayani Rungwe Andrew Mwendamanie akimshukuru Mkurungezi wa Tigo nyanda za juu kusini kwa kuwasogezea huduma ya malipo kwa njia ya Tigo. |
• Ni kupitia huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa ambayo ni salama na ya uhakika zaidi.
KAMPUNI ya Tigo Tanzania imeingia kwenye makubaliano na Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe ili kurahisisha malipo ya mazao yao kupitia simu maalumu kwaajili ya wakulima 8,000 katika Wilaya za Rungwe (Tukuyu), Busokelo na Kyela mkoani Mbeya.
Huduma hiyo ijulikanayo kama ‘Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa’ ni njia ya kinubinfu ya kutuma na kupokea pesa ambayo inayopatikana kupitia huduma ya kifedha ya Tigo, Tigo Pesa.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa, Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Aidan Komba alisema “Tunafuraha sana kuungana na Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe kupitia huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa ambayo itatoa suluhu la kudumu la malipo na mahitaji ya kila siku ya kifedha kwa wakulima wa chai.”
Akifafanua namna huduma hiyo inafanya kazi, Komba alisema kwanza wakulima wanatakiwa kujisajili kupitia Umoja huo ili kuweza kunufaika na huduma hiyo ambapo pia watapewa taarifa juu ya ukusanyaji, usafirishaji, minada na mauzo ya mazao yao.
Mara baada ya fedha za mauzo kuingizwa kwenye akaunti ya Chama (Umoja wa wakulima) Tigo Pesa kupitia huduma ya Malipo ya Chai itatuma pesa moja kwa moja kwa wakulima ambao wamesajiliwa kwenye huduma hiyo na watapata Ujumbe mfupi SMS papo hapo.
Baada ya kupokea fedha wakulima watakuwa na uhuru wa kutoa, kutuma au kufanya miamala mingine waipendayo kwa njia ya Tigo Pesa iliyo na mawakala kote nchini.
Mwenyekiti wa Umoja huo, Lebi Hudson alisema “Tunapenda kuwashukuru sana Tigo Tanzania kwa kuhakikisha Umoja wetu unaingia kwenye mfumo wa fedha kidigitali (cashless). Wakulima wengi walikuwa wamezoea kutembea na pesa taslimu njia ambayo si salama hasa kwa kipindi ambacho tunakuwa tumepokea malipo ya mazao yetu.”
Zaidi ya wakulima 8,000 kwa mara ya kwanza hawatakuwa na wasiwasi kuhusu kuhusu malipo ya mazao yao. Huduma hii itawapa uhuru wa kupokea pesa na kutoa mahala popote nchini na kuwawezesha kufanya miamala kupitia Tigo Pesa huduma ya Tigo yenye mtandao mpana na wenye mawakala nchi nzima.
--
No comments:
Post a Comment