MSHINDI WA DROO YA SHINDA UNG'ARISHE NYUMBA YAKO AKABIDHIWA ZAWADI YAKE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 8 February 2021

MSHINDI WA DROO YA SHINDA UNG'ARISHE NYUMBA YAKO AKABIDHIWA ZAWADI YAKE

 

Mwakilishi wa maduka ya GSM home Dodoma Latifa Sulemani akimkabidhi mfano wa hundi mwakilishi wa mshindi wa droo ya nne ya shinda na kung’arishe nyumba inayoendeshwa na kampuni ya GSM kupitia maduka yake ya GSM home, Neema Venance tukio lililofanyika jijini Dodoma.



Mwakilishi wa mshindi wa droo ya nne ya shinda na kung’arishe nyumba inayoendeshwa na kampuni ya GSM kupitia maduka yake ya GSM home, Shani Chwila wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GSM home mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.

MSHINDI wa droo ya nne ya shinda ung’arishe nyumba yako inayoendeshwa na Kampuni ya GSM Tanzania kupitia maduka yake ya GSM home amekabidhiwa zawadi yake ya bedroom set na kufanya idadi ya washindi ya droo hiyo kufikia wanne.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi mwakilishi wa GSM Dodoma Latifa Sulemani amesema droo hiyo iliendeshwa kwa kila mteja aliyefanya manunuzi ya kuanzia milioni moja (1,000,000) na kuendelea na kuingizwa katika droo na kuwa katika nafasi ya kushinda.

“Droo hii ilikuwa kila mteja wetu aliyefanya manunuzi ya kuanzia milioni moja tunamuingiza katika droo hii na anayebahatika anazawadiwa seti ya chumbani na tunashukuru na sisi Dodoma tumempata mshindi leo,” amesema Latifa.

Amesema mshindi huyo ni wa mwisho katika shindano hilo ambalo lilihusisha maduka manne ya GSM home ambayo ni GSM home Mlimani city, GSM home Mikocheni, GSM home Pugu na Dodoma ambapo jumla ya washindi wanne walipatikana na kukabidhiwa zawadi zao.

Aidha amebainisha kuwa katika maduka ya GSM kuna punguzo la bei kwa kila bidhaa ambapo punguzo lipo hadi asilimia 50 ya bidhaa zinazopatikana katika maduka ya GSM na kutaka wateja kuchangamkia fulsa hiyo kabla haijaisha.

Kwa upande wake mwakilishi wa mshindi wa droo ya shinda ung’arishe nyumba yako Shani Chwila, aliyemuwakilisha Neema Venance ambaye ndio mshindi wa droo hiyo amesema amekuwa mteja mzuri wa GSM hadi alipofanikiwa kushinda droo hiyo.

“Nashukuru nimeshinda nilifika katika duka la GSM home nikanunua samani na kujaza kuponi na hatimaye nikapigiwa simu kuwa nimeshinda na leo nimekuja hapa na kukabidhiwa zawadi niliyoshinda,” amesema Shani.

Ameongeza kuwa “Nawashauri wenzangu kununua bidhaa katika maduka ya GSM kwani bidhaa ni nzuri na zinaubora mkubwa kwa matumizi na zinabei ndogo,” amesema.



No comments:

Post a Comment