Nahodha wa timu ya TRA akiwa amebeba Kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu baada ya kuibuka washindi kwenye Michuano ya Shimuta |
Nahodha wa timu ya TRA akiwa amebeba Kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu baada ya kuibuka washindi kwenye Michuano ya Shimuta |
Meneja wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo |
TIMU ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa kwanza katika mchezo wa fainali wa mpira wa miguu katika Mashindano ya Shimuta 2020 baada ya kuibamiza timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mabao 2-0 ,uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
Katika mchezo ambao ulikuwa wa aina yake huku TRA wakionekana kucheza kwa umakini mkubwa na hivyo kupelekea kupiga pasi fupi fupi na ndefu hali ambayo iliwachanganya wapinzani wao na hivyo kujikuta wakipokea kipigo hicho.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kwamba ushindi kwao ulikuwa hauna kipigamizi kutokana na namna walivyokuwa wakizifunga timu nyengine wakati wa michuano hayo.
Alisema kutokana na ushindi huo umeonyesha kwamba walikuwa wamejiimarisha vilivyo baada ya mashindano yaliyopita mwaka jana kuishia mshindi wa pili lakini mwaka wakajiwekea malengo ya kuweza kupata ushindi huo.
"Kwa mwaka huu nasikia faraja zaidi kwa sababu tumetembeza kichapo mwanzo mwisho hamna timu imetufunga na ndio maana tumekuwa mabingwa kwa mpira wa miguu " alisema Owure.
Naye Mwenyekiti wa Michezo wa timu ya TRA Mohamed Salim amesema kuwa kutokata tamaa na kufanya mazoezi ndio Siri ya ushindi wa TRA kuwa mabingw wa Mpira wa miguu katika mashindano ya Shimuta2020.
Alisema kuwa wameshiriki mashindano hayo kwa mara ya tatu sasa kwa mara ya kwanza walishiriki mkoani Dodoma na kushika nafasi ya tatu na mara ya pili mwaka Jana hawakukata tamaa wakashiriki mkoani Mwanza na kushika nafasi pili na hatimae mwaka huu 2020 wamefika fainali na kuchukua ubingwa.
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wa pili kutoka kulia akimkabidhi
nahodha wa timu ya TRA Kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu baada ya
kuibuka washindi kwenye Michuano ya Shimuta |
No comments:
Post a Comment