CRDB BENKI YACHANGIA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 17 August 2020

CRDB BENKI YACHANGIA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI

Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa wananchi walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo leo wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam. 

 
 Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya Shilingi milioni 200 iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi tuzo iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB kutambua huduma zinazofanywa na taasisi hiyo wakati wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI.


Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam
Picha na JKCI.

No comments:

Post a Comment