Mashabiki wa timu ya Simba. |
Hivyo, Wizara imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa kuruhusu mechi kati ya timu ya Tanzania Prisons na Simba (Juni 28, 2020) kuchezwa na mashabiki baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kuthibitisha kwa maandishi kuwa watasimamia utaratibu wote wa Kanuni za Afya Michezoni kuzingatiwa wakati wa mchezo huo ikiwemo mashabiki kuingia wachache na kupangwa na kusimamiwa kukaa kwa kuachiana mita moja.
Pamoja na ahadi hiyo, iwapo kutakuwa na uvunjifu wowote wa taratibu uwanja huo utachukuliwa hatua kali zaidi ikiwemo kuzuiwa usitumike kabisa kwa michezo ya ligi kuu.
Aidha, Wizara inaendelea kuwakumbusha wadau wa michezo pamoja na mashabiki kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoasababishwa na virusi vya Corona na kusisitiza kuwa hatua zitaendelea kuchukuliwa kwa viwanja vitakavyokiuka Mwongozo wa Afya michezoni.
Imetolewa na; Shamimu Nyaki
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini.
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
No comments:
Post a Comment