RAIS JPM AFANYA KIKAO CHA NDANI NA RAIS WA ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 3 June 2020

RAIS JPM AFANYA KIKAO CHA NDANI NA RAIS WA ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2020 amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein Ikulu ya Chamwino   Dodoma leo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru  Ally Kakurwa wakifuraia jambo leo tarehe 03-06-2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akizungumza na wajenzi kutoka JKT mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa Ofisi za IKULU. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment