WASHAURIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAHABARI KUTEKELEZA MAJUKUMU KIPINDI CHA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 28 April 2020

WASHAURIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAHABARI KUTEKELEZA MAJUKUMU KIPINDI CHA CORONA

Mwanasheria na Wakili Maarufu nchini Albert Msando (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vitakasa mikono 100 na Barakoa 100 kwa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) makao makuu ya APC jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Club ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu akitoa neno la Ukaribisho kwa wageni Wakili Alberto Msando na familia yake waliofika kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Na Ahmed Mahmoud, Arusha


IMEELEZWA kuwa Waandishi wa habari nchini wapo kwenye kipindi kigumu cha kutekeleza majukumu yao wakati huu wa mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19 kiuchumi na wadau wametakiwa kujitokeza kusaidia kada hiyo ili iweze kutoa taarifa sahihi na kweli.

Kwa mujibu wa Mdau wa maendeleo jijini Arusha Mwanasheria Maarufu Albert Msando na mmiliki wa The Don ambaye ametoa Barakoa na vitakasa mikono kwa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) ikiwa ni kusaidia mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19.

Msando akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo amesema kuwa kada ya uandishi wa habari ni muhimu Sana kutoa Taarifa za Ugonjwa wa Covid 19 lakini wao wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa kutokana na changamoto zao kipindi hichi cha janga la Corona

Aidha alisema kuwa imekuwa shida Sana kupata taarifa sahihi za Ugonjwa huu huku hali ikiwa inazidi kuwa mbaya na kipindi hichi jamii inahitaji taarifa zaidi  ili kuiondoa kwenye taharuki ni muhimu kwao wanahabari kuwezeshwa hata nauli ya kutoka eneo moja kwenda jingine itaisaidia jamii kupata taarifa sahihi sio Bora taarifa.

Alisema kuwa ni muhimu kwa waandishi kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo husika na kuzitoa utaona ni Jambo dogo Ila kila moja amekuwa na taharuki kutaka kujua taarifa kupitia kwenu nanyi ni watu muhimu Sana ikitoka wataalamu wa Afya ni nyinyi.

"Wadau wajitokeze kusaidia kwani waandishi wa habari wapo katika wakati mgumu Sana Kiuchumi katika kipindi hiki Cha Ugonjwa wa Covid 19 na jamii inahitaji taarifa za hali ya Ugonjwa huo huku waandishi wakiwa taabani kiuchumi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku," alisisitiza.

Aliwataka waandishi wa habari kusema ukweli kuhusu idadi ya watu wanaokufa waliopata Ugonjwa wa Covid 19 kwani jamii inapata taarifa sahihi kutoka kwao hivyo Amewataka kutumia uwezo wao wote na kufanya kazi hiyo kwa weledi. Aliwakumbusha wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia waandishi wa habari ili waweze kuwapatia wananchi taarifa za kina na sahihi kuhusiana na janga hili ili kuondoa taaruki miongoni mwa jamii.

Naye Mwenyekiti wa chama cha wa ndishi wa habari Mkoa wa Arusha,Claud Gwandu alimpongeza Mdau huyo kwa msaada wake huo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia kada hiyo.

Alimshukuru Mdau huyo kuikumbuka kada hiyo na kuona umuhimu wao wa kuwapatia vitendea kazi hivyo kipindi hichi cha janga la Corona ambavyo vitawafanya kufanya kazi zao wakati huu wa janga la Ugonjwa wa Covid 19.

No comments:

Post a Comment