WAKILI GAUDIOSUS ISHENGOMA AFARIKI DUNIA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 28 April 2020

WAKILI GAUDIOSUS ISHENGOMA AFARIKI DUNIA...!


Na Happiness Katabazi

WAKILI Ishengoma wa FB Attorneys  "  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Ishengoma enzi za uhai wake alikuwa Mwana Yanga kindakindaki" ni miongoni mwa mawakili maarufu nchini na baadhi ya mawakili wenzake wamekuwa wakimuelezea kuwa ni mzuri Sana katika kesi za jinai.

Kwa wale tuliofuatulia kesi maarufu ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar Es Salaam (ACP) - Abdallah Zombe na wenzake toka kesi hii ilipofunguliwa kwa Mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam.

Tulimshuhudia Wakili Ishengoma ambaye yeye alikuwa akimtetea aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Wilaya Kinondoni, Christopher Bageni kumnusuru na hatia ya kesi ya mauji na  mwaka aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Salum Massati, Agosti Mwaka 2009 aliwaachilia huru washitakiwa wote katika kesi hiyo ya wafanyabiashara wa nne wa Mahenge mkoani Morogoro kwa maelezo kwamba Zombe na wenzake siyo waliowaua wafanyabiashara na akaliamuru Jeshi la Polisi likawasake wauaji.

Lakini upande wa jamhuri haukuridhishwa na hukumu ya Mahakama Kuu, ukakata Rufaa Mahakama ya rufani na katika ngazi ya Mahakama ya Rufani, Bageni alikuwa hatetewi Tena na Wakili Ishengoma alikuwa anatetewa na Wakili maarufu wa Kujitegemea Majura Magafu na Mahakama ya Rufani Septemba Mwaka 2016 ikamkuta Bageni peke yake na kosa la kuua kwa kukusudia na ikamuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Mbali na kesi hiyo maarufu Kama "kesi ya Zombe" , Wakili Ishengoma   Aliwahi kumwakilisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa soka enzi hizo kikitambulika Kama FAT Sasa hivi TFF , Ismail Aden Rage ambaye yeye na Mwenyekiti wa FAT , Muhidin Ndolanga ,Mhasibu Seleki na mfanyabiashara Speciouza Lugazia ambapo aliyekuwa  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu ambaye hivi Sasa ni marehemu Suma Seme,Mwaka 2005  alimuhukumu Rage kwenda jela miaka mitatu .

Baada ya kumtia hatiani kwa kosa  la wizi wa  fedha taslimu na mipira 50 Kati ya 600 Mali ya FAT alidaiwa kuyatenda Mwaka 1999. Miezi michache baada ya hukumu hiyo kutolewa ,Rais Benjamin Mkapa kabla yakumaliza kipindi chake cha miaka kumi madarakani Mwaka 2005 alitoa msamaha kwa wafungwa ambapo Rage alinufaika na msamahama huo.

Lakini Hakimu Seme alimtia hatiani Rage kwa Makosa yaliyokuwa yakimkabili na akaenda kutumia adhabu yake gerezani akakata rufaa mahakama Kuu na hatimaye mahakama ya Rufani nchini akiwakilishwa na Wakili  Ishengoma ,ambapo jopo la majaji watatu Jaji Damian Lubuva, John Mrosso  na Mbarouk Mbarouk  walimuachiri huru  Rage na kutengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyokuwa imemuhukumu kifungo Cha jela miaka mitatu .

Binafsi mwisho wa kuzungumza na kuibadilisha nae taarifa za kifo Cha Wakili John Mhimili  Mapinduzi aliyefariki Aprili Mosi Mwaka huu katika Hospital ya Jeshi Lugalo ilikuwa ni April Mosi, mbili na tatu kwanilikuwa namrushia taarifa za kilichokuwa kikijiri katika msiba huo wa Mwanasheria mwenzetu na mpendwa na aliniambia Yuko mbali hawezi kuwahi kuaga mwili wa Wakili Mapinduzi akaniomba nimwakilishe akasema ameumizwa Sana na kifo Cha Mapinduzi.

Wakili Ishengoma alikuwa ni miongoni mwa vyanzo vyangu vya habari   enzi nikiwa mwandishi wa habari za mahakamani kabla sijawa Mwanasheria. Ikumbukwe kwamba Ishengoma ambaye ni Shabiki wa Yanga  kabla ya kuwa Wakili wa Kujitegemea Aliwahi kuwa Wakili wa Serikali kwa miaka nane akaacha kazi hiyo akaamua kuwa Wakili wa kujitegemea .

Sote tuliokuwa karibu na Wakili Ishengoma nakufanya nae kazi mtakubaliana namimi kuwa ni mtu  aliyependa  utani, kuhoji, haki na kucheka na mchapakazi.

Hakika kifo kaka Ishengoma kimenikumbusha enzi zile za mawakili maarufu nchini ambao mbali ya kuwa mawakili Lakini walikuwa ni mashabiki wa Timu za Simba na Yanga wa kutupwa Hadi ilikuwa raha mahakamani kusikiliza kesi za Simba au Yanga zilizokuwa zikifunguliwa mahakamani nao Kama mawakili walikuwa wakiziwakilisha Timu zao makamani.

Genge la mawakili hao ni Ishengoma (Marehemu), Theonest  Rutashoborwa(Marehemu) , Martin Matunda (Marehemu) , na Alex Mgongolwa na Shaban Madega (Kiongozi wa Yanga mstaafu).

Kwa upande wa mawakili wakereketwa  mashabiki wa Simba Shabiki  ni Wakili maarufu nchini Peter Swai ambaye huyu mara zote pindi timu ya Simba ikishitakiwa amekuwa mstari wa mbele kwenda kuiwakilisha mahakamani, Kassim Nyangarika ambaye kwasasa ni Jaji , Wakili Ngatunga.

Kifo cha Kaka yangu na Mwanasheria mwenzangu Ishengoma kimeniuma sana.

Mungu aiweke roho ya Wakili Gaudiosus Ishengoma mahali panapostahili.

Mwandishi wa makala hii ni Mwandishi wa Habari na Mwanasheria.

0716 774494.

No comments:

Post a Comment