MATUKIO PICHA : KARUME DAY - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 7 April 2020

MATUKIO PICHA : KARUME DAY

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mihayo Juma Nhunga (kushoto), wakati akiwasili kwenye uwanja wa Abeid Amani Karume, kumwakilisha Rais Magufuli, kwenye dua ya kumuombea aliyekua Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, katika kumbukizi ya kifo chake, Zanzibar Aprili 7, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, wakiomba dua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, kwenye dua ya kumuombea muasisi huyo, iliyofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, katika kumbukizi ya kifo chake, Zanzibar Aprili 7, 2020. Waziri Mkuu amemwakilisha Rais Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, baada ya dua ya Muasisi na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, katika kumbukizi ya kifo chake, Zanzibar Aprili 7, 2020 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Karume, akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, wakiomba dua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, baada ya dua ya Muasisi na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, katika kumbukizi ya kifo chake, Zanzibar Aprili 7, 2020 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

No comments:

Post a Comment