Mgonjwa wa Corona akiwa katika mazoezi. |
UGONJWA wa Covid-19 ulijitokeza 2019, lakini tayari kuna ishara kwamba inaweza kuchukua muda mrefu kwa baadhi ya wagonjwa kupona kabisa.
Muda wa mgonjwa kupona itategemea na hali yake yaani vile anavyoendelea. Dalili kwa baadhi ya watu zitaanza kujitokeza kwa haraka ikilinganishwa na wengine lakini pia ugonjwa wa virusi vya corona unaweza kusababisha matatizo makubwa kwa wengine.
Umri, jinsia na matatizo mengine ya afya yote yanaongeza hatari ya kuwa mgonjwa zaidi kwasababu ya Covid-19. Kadiri unavyoendelea kupata matibabu ya kina, na muda utakaokuwa unapokea matibabu hayo, kunachangia uwezekano mkubwa wa mgonjwa kuchukua mrefu kupona.
Watu wengi wanaopata ugonjwa wa Covid-19, dalili za msingi pekee ndo zitakazojitokeza. Lakini pia wanaweza kuhisi mwili kuuma, uchovu, vodonda vya koo na kuumwa na kichwa.
Mara ya kwanza kikohozi huwa ni kikavu, lakini baadhi ya watu hatimae wataanza kukohoa na kutoa makohozi yenye seli zilizokufa kutoka kwenye mapafu zilizouliwa na virusi.
Dalili hizi zinaweza kutibiwa kwa kupumzika vizuri, kunywa maji mengi na dawa za kuondoa maumivu. Watu wenye dalili za wastani, wanatarajiwa kupata afueni ya haraka.
Homa inastahili kupungua chini ya wiki moja, ingawa kikohozi huenda kikaendelea. Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa takwimu za China unaonesha kwamba kwa wastani inachukua wiki mbili mtu kuanza kupona.
Kwa baadhi ya watu, hali zao zinaweza kuendelea kuwa mbaya zaidi. Hili mara nyingi hutokea kati ya siku 7 hadi 10 kipindi ambacho mtu atakuwa amepata maambukizi.
Manesi wakiwa na mgonjwa wa virusi vya Covid 19. |
Pia hali ya mgonjwa inaweza kubadilika ghafla. Kupata matatizo ya kupumua na mapafu kuanza kufura. Hii ni kwasababu ingawa mfumo wa kinga wa mwili unajaribu kukabiliana na matatizo hayo - hali inakuwa mbaya huku mwili ukiendelea kudhohofika. Baadhi ya watu watahitaji kuwa hospitali ili kuweza kuwekewa oksijeni.
Daktari, Sarah Jarvis anasema: "Kwa matatizo ya kupumua huenda ikachukua muda kudhibitika…mwili unaendelea kudhohofika na mapafu kufura."
Anasema kwamba mgonjwa mwenye matatizo hayo anaweza kuchukua wiki 2 hadi 8 kupona kipindi hicho akiwa anapitia maumivu makali.
Je inakuwaje mtu akihitajika kuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kwamba mtu mmoja kati ya 20 atahitaji huduma ya wagonjwa mahututi, ambayo inaweza kujumuisha mtu kudungwa sindano ya kulala fofofo na kuwekwa kwenye mashine ya kupumua.
Itachukua muda mtu kupona mgonjwa akiwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi bila kuzingatia ugonjwa alionao. Baada ya kupata nafuu, mgonjwa huhamishwa hadi chumba cha wagonjwa wa kawaida kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Daktari Alison Pittard, mkuu wa kitivo cha wagonjwa mahututi, anasema inaweza kuchukua miezi 12 hadi 18 kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupata huduma yoyote ile ya wagonjwa mahututi.
Kuwa hospitali kitandani tu kwa muda mrefu, kunaweza kusababisha matatizo ya misuli. Wagonjwa watakuwa dhaifu na misuli yao itachukua muda mrefu kurejea tena katika hali ya kawaida. Baadhi ya watu watahitaji tiba ya kurekebisha viungo ili kuweza kutembea tena.
Kwasababu ya kile kinachoendelea katika chumba cha wagonjwa mahututi, kuna uwezekano akapata matatizo ya kuchanganyikiwa na ya akili. Kuna taarifa kutoka China na Italia kwamba mwili mzima wa mgonjwa huwa dhaifu, matatizo ya kupumua, kukohoa kunakoendelea pamoja na kutaka kulala tu.
"Tunafahamu kwamba kuna wagonjwa wanaochukua muda mrefu kupona wengine hata miezi kadhaa."
Lakini ni vigumu kuchukulia kwamba hali kwa wagonjwa wote huwa hivyo. Baadhi huchukua muda mfupi tu kuwa katika mashine ya kupumua ilihali wengine inawachukua hadi wiki mbili.
Hadi kufikia sasa hilo halijafahamika, lakini inawezekana kuchunguza hali ya mgonjwa. Wenye matatizo makubwa ya kupumua kwa wale ambao kinga yao ya mwili itadhohofika, ugonjwa huo utadhuru mapafu.
"Kuna data inayoonesha kwamba hata baada ya miaka mitano, kuna uwezekano baadhi ya watu wakaendelea kuwa na matatizo ya afya ya akili," amesema bwana Twose.
Daktari James Gill, na mhadhiri wa chuo cha tiba cha Warwick, anasema kwamba wagonjwa pia wanahitaji usaidizi wa afya ya akili ili kuweza kupona kwa haraka.
"Ikiwa una matatizo ya kupumua, daktari anasema 'Tunahitaji kukuweka kwa mashine ya kupumua. Tutakudunga sindano ya kulala fofofo. Pengine ungependa kuaga familia na rafiki zako?'.
Hapo kunaendelea kuwa na uwezekano kuwa hata wagonjwa wenye dalili za wastani, wanaweza kupata matatizo ya afya ya muda mrefu kama uchovu.
Kupata takwimu sahihi ni vigumu. Kufikia Aprili 15, Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilisema karibia watu 500,000 wamepona kati ya milioni 2 waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona.
Lakini kila nchi inatumia njia yake tofauti. Kuna maadhi ya mataifa ambayo hayachapishi idadi ya waliopona na takwimu za wengi wenye dalili za wastahi hazirekodiwi.
Je, mtu aliyeugua ugonjwa wa corona anaweza kupata maambukizi tena?
Virusi hivi vipya vya corona , vinaweza kukusababisha mtu uugue na wengi ni watu wenye shida ya mapafu.
Lakini virusi hivi vipya hakuna ambaye ana kinga dhidi yake. Hivyo haijalishi kama uliugua mwanzo au la.
Aidha shirika la afya duniani limesema kuwa kabla ya miezi 18 kupita chanjo ya corona itakuwa imepatikana.
-BBC
No comments:
Post a Comment