WAZIRI KAMWELWE AKAGUA ATHARI ZA MIUNDOMBINU BARABARA NA MADARAJA MIKOA YA MOROGORO NA IRINGA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 19 March 2020

WAZIRI KAMWELWE AKAGUA ATHARI ZA MIUNDOMBINU BARABARA NA MADARAJA MIKOA YA MOROGORO NA IRINGA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isaack Kamwelwe (katikati) akiwa katika ziara yake kukagua ukarabati wa kingo za Daraja la Ruaha Mkuu, pamoja na kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Morogoro na Iringa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isaack Kamwelwe (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji akiwa ziarani kukagua ukarabati wa kingo za Daraja la Ruaha Mkuu, pamoja na kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Morogoro na Iringa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isaack Kamwelwe (katikati) akiwa katika ziara yake kukagua ukarabati wa kingo za Daraja la Ruaha Mkuu, pamoja na kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Morogoro na Iringa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Muonekano wa baadhi ya madarajaa aaliyoyakagua Mh Waaziri.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isaack Kamwelwe amekagua ukarabati wa kingo za Daraja la Ruaha Mkuu na kuutaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Morogoro kuimarisha usalama wa daraja hilo ili lipitike wakati wote.

Katika ziara hiyo, Waziri Kamwelwe amewataka mameneja wote wa TANROADS nchi nzima kukagua na kuimarisha madaraja yote katika maeneo yao ili kuepuka maafa katika kipindi hiki cha mvua.

"...Natoa siku saba kwa mameneja wote nchini kuhakikisha barabara za lami zinazibwa mashimo," alisema Waziri Kamwelwe. Waziri Kamwelwe anaendelea na ziara ya kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Morogoro na Iringa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Ambapo alikagua athari za mafuriko katika Daraja la Kidatu kwenye Mto Ruaha Mkuu mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi akizungumza katika ziara hiyo, alimwakikishia Waziri Kamwelwe kuwa eneo lake wamejipanga kushirikiana na TANROADS kuhakikisha usalama wa miundombinu wilayani humo unaimarishwa.

Aidha Mhe. Waziri Kamwelwe amekagua ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara yenye urefu wa kilometa 67 inayojengwa na mkandarasi RCC na kumtaka kuongeza kasi katika ujenzi huo.

No comments:

Post a Comment