MAASKOFU ANGLIKANA WAITAKA JAMII KUUNGANA NA JUHUDI ZA SERIKALI KUKABILIANA NA COVD 19 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 19 March 2020

MAASKOFU ANGLIKANA WAITAKA JAMII KUUNGANA NA JUHUDI ZA SERIKALI KUKABILIANA NA COVD 19

Askofu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt.Mahimbo Mndolwa akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha

KATIKA kukabiliana na ugonjwa wa corona nchini ,kanisa la Anglikana limetangaza kuongeza ibada zake katika makanisa yake yote ili kuondoa msongamano ambao ungeweza kusababisha maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

Akitoa tamko hilo jijini Arusha mbele ya maskofu 28 wa dayosisi za kanisa hilo, Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini Tanzania,ambaye pia ni Askofu wa dayosisi ya Tanga,Askofu Dokta Maimbo Mndolwa alisema kuwa,kama kanisa wamejipanga kuendelea kuunga mkono jitihada zote za serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa kushirikiana na wananchi na waumini wa kanisa hilo.

Askofu Mndolwa alisema kuwa ,kanisa hilo limejipanga kufanya ibada maalumu za mara kwa mara katika dayosisi zake zote zioatazo 28 bara na visiwani ,jumuiya na familia kwa ajili ya kumwomba Mungu kutuepusha na ugonjwa huo usiendelee kusambaa zaidi hapa nchini.

Alisema kuwa,wanaishauri serikali kuhimiza vyombo vya usafiri kuchukua hatua za tahadhari ikiwemo kunyunyiza dawa kwenye vyombo vya usafiri kama mabasi,ndege na maeneo ya usafiri.

"Tunaomba serikali kusimamia mfumuko wa bei katika bidhaa muhimu na vyakula katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa huo wa Corona.""alisema Askofu.

Aliongeza kuwa,wao kama kanisa wana imani kubwa kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu ,hivyo wanaendelea kupiga goti kutafuta uso wa Mungu katika kipindi hiki Cha kwaresma ili asikie Sala zetu na kuturehemu ili kutuepusha na gonjwa hilo.

Alisema kuwa ,kanisa linaelekeza kuwa kila dayosisi itenge siku maalumu ya maombi kuanzia machi 19 kwa ajili ya kuombea ugonjwa huo ili Mungu aweze kuingilia Kati.

" Tumepanga kuziongeza ibada zetu ili kupunguza msongamano wa waumini wetu katika makanisa yetu yote nchini "alisema askafu.

Askofu aliongeza kuwa ,kama kanisa kwa pamoja siku ya ijumaa kuu itakuwa siku ya ibada ya pamoja kanisa la Anglikana Tanzania kwa ajili ya kuombea Taifa letu dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona.

"Tutaendelea kuwaombea wafanyakazi wote wanaotoa huduma kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Corona ili Mungu awaepushe na magonjwa hayo sambamba na kuwapa uvumilivu katika kuwahudumia ."alisema Askofu.

Aidha ugonjwa huo ulianzia nchini China desemba 2019 na kuenea sehemu mbalimbali hapa duniani,ambapo mpaka sasa hivi kwa Tanzania kuna wagonjwa wapatao sita waliothibitishwa na serikali kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

No comments:

Post a Comment