NMB: HUDUMA YA BIMA KUPITIA BENKI HUKUZA BIASHARA ENDELEVU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 19 March 2020

NMB: HUDUMA YA BIMA KUPITIA BENKI HUKUZA BIASHARA ENDELEVU

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati - Filbert Mponzi akizungumza na wateja waliohudhuria mkutano wa NMB Business Club kupata maoni yao kuhusu huduma na bidhaa za NMB.

Meneja wa Mikopo ya Nyumba NMB - Miranda Lutege akielezea mikopo ya nyumba wakati wa mkutano wa NMB Business Club.

Meneja Mwandamizi wa Bima wa Benki ya NMB Martine Massawe akielezea kuhusu Bima ‘Bancassuarance’ wakati wa mkutano wa NMB Business Club.

BENKI
ya NMB imesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kukata bima ya biashara zao ili ziwe endelevu kwa kuzilinda dhidi ya hatari (risks) zinazoweza kujitokeza.
Akizungumza katika semina iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 300 wanaounda Klabu ya Biashara ‘NMB Business Club’ ya Mkoa wa Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati wa NMB - Filbert Mponzi, alisema kuwa biashara hukabiliwa na hatari (risk) mbalimbali ambazo kinga yake ni kuzikatia bima. Majanga kama moto, wizi na mafuriko ni baadhi ya hatari zinazozikabili biashara na kudumaza ukuaji endelevu wake.
Ikiwa na matawi 225 nchini kote, NMB inayo nafasi bora ya kufikisha huduma za bima kwa watu wote (wateja wake na wasio wateja wake) popote walipo.
Benki ya NMB inatoa huduma za bima (Bancassurance) katika matawi yake yote 225 nchini kote kupitia ushirikiano wake na kampuni za bima za Sanlam, UAP, Shirika la Bima la Taifa (National Insurance Corporation - NIC), Jubilee, Shirika la Bima la Zanzibar (Zanzibar Insurance Corporation – ZIC) na Reliance.
Kwa ushirikiano na kampuni tajwa, matawi ya Benki ya NMB hutoa huduma za bima za magari, afya, mali za thamani, maisha, hatifungani na kilimo.
Mponzi alikuwa akizungumza katika semina iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 300 wanaounda Klabu ya Biashara ‘NMB Business Club’ ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kwa kupitia huduma ya bima kupitia benki (Bancassurance), Watanzania wanaweza kukata bima na kuomba malipo ya bima pindi hatari zinapojitokeza kupitia matawi yote na NMB nchini kote.
Vilabu vya Biashara vya NMB huwakutanisha pamoja wafanyabiashara wadogo na wa kati   ambao hupata nafasi ya kuelimishwa juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara zao.
Meneja mwandamizi wa huduma ya bima kupitia benki wa NMB, Martine Massawe, aliwaambia washiriki wa semina hiyo kuwa uwepo wa matawi ya NMB karibu na maeneo yao kunatoa fursa ya wao kupata huduma za bima kwa karibu zaidi.
Mjasiriamali na mshiriki wa semina hiyo ambaye biashara yake iliathiriwa na moto uliounguza sehemu ya Soko la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam hivu karubuni - Godwin Rwechungura alitoa ushuhuda wa jinsi Benki ya NMB ilivyomhakikishia kupata fidia ya hasara aliyoipata.
Naye meneja mwandamizi wa huduma za benki kwa njia ya kidijitali wa Benki ya NMB, Tito Mangesho alisema mbali na huduma za bima kupitia benki, taasisi hiyo ya fedha pia hutoa huduma za NMB Mkononi, Mastercard QR Code na nyingine nyingi kupitia kadi ambazo kwa pamoja husaidia kuboresha ufanisi katika biashara.
Kupitia NMB Mkononi, mteja huweza kufanya miamala ya kifedha popote pale alipo kwa kupitia simu ya mkononi.

Mteja pia anaweza kufanya malipo kama vile ya kodi na tozo mbalimbali za serikali moja kwa moja kupitia simu ya mkononi.

No comments:

Post a Comment