Moja kati ya maeneo ya uzalishaji wa miche ya miti katika shamba la miti ya sao hill kwa ajili kuendelea kuipanda katika shamba hilo na kwa baadhi ya wananchi wanaolizunguka shamba hiloMoja kati ya eneo la shamba la miti la Sao hill katika wilaya ya Mufindi
NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
WAKALA wa Misitu Tanzania TFS kupitisha Shamba la Miti Sao Hill Wilayani Mufindi
mkoani Iringa Limewahimiza wananchi kuendelea kuitunza misitu iliyopo katika
maeneo yao na kuitumia kuwa fursa ya kiuchumi kwa kizazi cha sasa na baadae.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea Siku ya Misitu Duniani ambayo
huadhimishwa Tarehe 21 ya mwezi wa Tatu ya kila mwaka, Meneja wa Shamba la Miti
Sao hill Juma Mseti amesema utunzaji wa misitu hiyo utaendelea kuchochea
maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa, pamoja na kutoa ajira mbalimbali kwa wananchi
wanaozunguka maeneo ya misitu hiyo.
Alisema
kuelekea maadhimisho hayo wameendelea kusisitiza juu ya utanzanji wa mazingira
na uhifadhi wa misitu ikiwemo ya Sao hill kwa lengo la kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi kwa manufaa ya jamii nzima.
Mseti
alizungumzia juu ya faida za uhifadhi wa misitu meneja Juma Mseti amesema licha
ya kuwa chanzo cha ajira kwa jamii, pia misitu ni sehemu ya makazi ya wanyama, husaidia
katika ulinzi wa vyanzo vya maji pamoja na kuzuia mmomonyoko wa Udongo.
“Maadhimisho
ya siku ya misitu ufanyika Machi 21 kila
mwaka huku nchi mbalimbali Duniani zikihimizwa kuendeleza juhudi za kitaifa na kimataifa ili
kuandaa na kushiriki katika shughuli zinazohusika na misitu pamoja na miti,
kama vile kampeni ya kupanda miti pamoja na midahalo kuhusu misitu. Siku hii
huadhimishwa kwa ajili ya kuwafanya watu waelewe umuhimu wa aina zote za misitu
duniani, ikiwemo jukumu lake katika mabadiliko ya tabia nchi” alisema Mseti
Tamko
la Umoja wa Mataifa linaiomba Sekretarieti ya Jumuiko la Umoja wa Mataifa juu
ya Misitu (UNFF), kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO), kufanikisha utekelezaji wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Misitu, kwa kushirikiana na Serikali, pamoja na wadau wa Masuala ya Misitu wakiwamo Sao hill na taasisi
mbalimbali
Kauli
mbiu iliyochaguliwa kwa mwaka 2020 juu ya maadhimisho ya siku ya misitu Dunia "MISITU
BIOANUWAI NI TUNU NA TUILINDE"
No comments:
Post a Comment