Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM, Mhashamu Yuda Thadei Ruwa'ichi. |
WAH. Mapadri, Mashemasi, Watawa na Waamini wote, Kristo. Napenda kuwafahamisha maagizo yaliyotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM, Mhashamu Yuda Thadei Ruwa'ichi, Leo tarehe 17 Machi 2020 Maagizo hayo yanalenga kujihadhari na ugonjwa wa CORONA. Nayo ni:
1. Kutopeana Amani kwa mikono wakati wa Misa.
2. Kupokea Ekaristi Takatifu kwa mikono tu na siyo kwa midomo. Ila umakini uhimizwe ili Yesu anayebaki mikononi katika vipande vidogo vidogo, ASITUPWE CHINI
3. Kutotumia Maji ya Baraka ya Kuchovya. Sehemu zote yalimowekwa (Milangoni MAKANISANI) YAKAUSHWE. Katika Adhimisho, Kiongozi wa ibada anaweza kuwanyunyizia Waamini maji ya Baraka.
4. Tunaombwa kuchukua kila tahadhari ili kujiepusha na ugonjwa huu.
5. Kufuata kwa makini maelekezo yaliyotolewa na Serikali katika kuudhibiti ugonjwa huu.
N.B: maelekezo mengine yatatolewa taratibu
Pd. Frank Mtavangu
Katibu-Jimbo
No comments:
Post a Comment