MACHAFUKO: RAIA BURKINA FASO KUPATIWA SILAHA KUPAMBANA NA WANAMGAMBO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 3 February 2020

MACHAFUKO: RAIA BURKINA FASO KUPATIWA SILAHA KUPAMBANA NA WANAMGAMBO



Jeshi la Burkina Faso linaungwa mkono na vikosi vya Ufaransa ambao pia wako katika baadhi ya sehemu ya Sahel

MAAFISA nchini Burkina Faso, wanahangaika kukabiliana na ongezeko la wimbi la mashambulio ya wanamgambo wa kiislamu yanayoongezeka ambayo yanaathiri kanda hiyo, wamepanga kuwapatia raia silaha.

Serikali ya Burkinabe inakabiliwa na shinikizo la kuchukua hatua kujaribu kudhibiti wanamgambo.
Mwezi Januari pekee, watu wapata 60 waliuawa katika mashambulio manne tofauti kaskazini mwa nchi hiyo.

Hivi karibuni wabunge walipiga kura kwa kauli moja kuuunga mkono kuwapatia raia silaha, hatua ambayo wanasema itasaidia kupambana na makundi yenye silaha. Inatarajiwa kusainiwa kuwa sharia.

Mashambulio ya wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya al-Qaeda na Islamic State yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, na kusababisha , zaidi ya watu milioni moja kuyakimbia makazi yao.

Wakosoaji wa wamehoji ikiwa hatu mpya itawafanya watu waumie, lakini serikali inasisitiza kuwa watu watakaojitolea kuwa na silaha ni muhimu kwani watasaidia kumaliza kusambaa kwa ghasia.

Je ni kwanini raia wanahusishwa ?

Sheria inasema kuwa uwezo wa jeshi wa kupambana na wanamgambo hautoshi kutokana na idadi yao kuwa ndogo na kuna ukosefu wa mafunzo yanayofaa.

"Kwasababu ya tisho linaloendelea, watu wameelezea utashi wao wa kushiriki kikamilifu katika kuilinda nchi yao," ilisema.

Lakini huu sio ushahidi wa udhaifu wa jeshi, ilisisitiza. Akizungumza na BBC waziri wa mawasiliano Remi Dandjinou aliwafananisha watakaojitolea kupewa silaha kama kikosi cha kujilinda cha Ufaransa kilichokuwepo wakati wa uvamizi wa Ujerumani wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia.

Lakini kuna hofu kwamba hatua mpya kuchoche zaidi mzozo wa kikabila na kuchochea uhasama baina jami za wawindaji na wakulima.

"Vikosi vya usalama vya Burkinafaso vinajilazimisha kuhusika katika ukatili mbaya dhidi ya washukiwa," Corinne Dufka kutoka Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch aliiambia BBC. "Hiyo ndio maana kutoa wajibu wowote wa kujilinda kwa raia wenye silaha ni tatizo."

"Inaweza kuchochea uhasama wa kijamii na kusababisha ukiukaji mkubwa haki za binadamu, ambao unaweza kuwasukuma zaidi watu kuingia mikononi mwa makundi ya Jihad ."

Serikali ya Burkina Faso awali ilikana madai ya kuenea kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Ni nani atakayepewa silaha?

Raia yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kukubaliwa kupewa mafunzo na hakuna umri wa ukomo. Lakini kupewa mafunzo haiwezi kuwa ni sehemu ya kundi lolote la kisiasa.

Wanaojitolea kupewa silaha lazima wawe wazalendo na waaminifu wenye "moyo wa kujitolea " mkiwemo " kujitolea muhanga kwa ajili ya nchi", kwa mujibu wa sheria iliyoungwa mkono na Wabunge.

Lakini, baada ya kupitishwa,Waziri wa Ulinzi Cheriff Sy alisisitiza kuwa mafunzo hayawezi kutumiwa kama " chakula cha kila mtu".

Vijiji kama hiki Kaskazini mwa Burkina Faso viko kwenye hatari ya kupatwa na machafuko

Utoaji wa silaha utafanyika kwa kiwango cha ngazi za mwanzo za utawala ambapo viongozi wa vijiji watasimamiwa na jeshi.

Lakini watakaojitolea hawatakua njiani kuidhinishwa kama makundi ya kujilinda, yanayowajumuisha watu ambao wakati mwingine wanajulikana kama makundi ya kujilinda.

Katika nchi ya Burkina Faso, kama ilivyo kwa Mali na Nigeria, raia wamejihami kulinda nyumba zao, na wakati mwingine, wamekua wakijipata katika makosa.

Makundi haya ya kujilinda hayaongozwi na mamlaka. Mara nyingi huwa yanaundwa kulingana na makabila na yamekuwa yakilenga jamii hasimu.

Moja ya hofu zilizojitokeza ni kwamba sehemu za nchi -hadi theluthi moja kwa kiwango fulani-wanaaminiwa kuwa chini ya udhibiti wa makundi ya wanamgambo, na hivyo kuyafanya kuwa hatari sana na vigumu kutoa silaha katika maeneo hayo.

Maeneo ya mipaka kaskazini na kaskazini-mashariki inayopakana na Mali na Niger yamekabiliwa na mashambulio zaidi, lakini yameongezeka pia sana katoka maeneo ya mipaka ya kusini.



Je watakaojitolea watapata mafunzo gani?

Haijawa wazi ni lini watakaopewa silaha watapata mafunzo na ikiwa watu watakua makini kupata mafunzo.

Sheria inasema kuwa walau watu 10 wanatakiwa kujiandikisha kupokea mafunzo kwa kila kijiji au eneo la makazi.

Watakapopewa mafunzo, watapata mafunzo ya siku 14, ambayo yatajumuisha jinsi ya kutunza silaha , mbimnu za kimsingi za kivita, sharia za nidhamu na mafunzo ya kiraia na kimaadili.

Haijabainika ni nani atakayetoa mafunzo na ikiwa yatakua yakifuatiliwa au la.

Baada ya kupewa mafunzo , waliohitimu watapewa silaha, pamoja na vifaa vya uchunguzi na mawasiliano. Lakini hawatapewa sare.

Huku watakaojitokeza , ambao wanatarajiwa kusaini mkataba kwa walau mwaka mmoja, hawatalipwa, makundi hayo yatapokea msaada wa kifedha kutoka kwa serikali kwa ajili ya vifaa na gharama nyingine za kikazi . Pia wanaruhusiwa kupokea misaada.

Watalipiwa garama za matibabu iwapo watajeruhiwa na kulipwa fidia pale watakapopata majeraha ya kudumu. Gharama za mazishi zitalipwa kwa wale watakaokufa katika mapambano

Kitaifa, wizara ya ulinzi itasimami kazi ya kikosi cha kiraia, lakini katika maeneo ya vijijini watasimamiwa na machifu wa vijiji.

Kazi yao ni ipi?

Watakaojitolea wanatarajiwa kuwepo wakati wote vijijini mwao.

Wanatarajiwa kusaidia kazi za jeshi na polisi , kusaidia kuvilinda vijiji au wilaya.

Hii inaweza kuwa ni pamoja na kufanya uchunguzi na kutoa taarifa za kijasusi kwa jeshi lakini hawaruhusiwi kufanya shughuli za polisi.

Watakaojitolea wanatarajiwa kuheshimu sharia ya maadili , ambayo kwa sasa haijatangazwa kwa Umma.


-BBC

No comments:

Post a Comment