WATANZANIA wameaswa kuendelea kuchukua hatua na kufuata
maelekezo ya wataalamu wa Afya sanjari na kuendelea kutoa elimu ya kuepuka
maambukizi mapya ya ugonjwa wa covid 19.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa
Arusha David Lyamongi wakati akikabidhi vifaa vya kujikinga na maambukizi ya
Ugonjwa wa Covid 19 kwa mawakala wa uuzaji wa Pembejeo mkoani humo kwenye hafla
iliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa kipindi hicho maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa
yamepungua nchini elimu juu ya janga hilo inatakiwa kuendelea kutolewa ili
kuweza kuutokomeza kabisa ugonjwa huo nchini na kuwashukuru kampuni ya YARA
kuona umuhimu wa kuwakumbuka wateja wao wakiwamo wakulima.
“Sote ni mashahidi wakulima ni kada muhimu sana ndio maana
mh.Rais wetu aliliona hilo na kuacha kutufungia ndani ilituendelee na
uzalishaji kipinchi chote cha janga la ugonjwa huu hivyo tuonyeshe kuunga mkono
kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya ili kuweza kuutokomeza
nchini mwetu”
Awali Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt.Wilson Sichalwe
alisema kuwa elimu zaidi inahitajika kwa wananchi sanjari na utoaji vifaa hivyo
ujumbe uendelee kutolewa ilikuendeleza mapambano ya kuuondoa hapa nchini.
Alisema mkoa umejipanga kuhakikisha unaendelea kutoa elimu
kwa umma na kuendelea kuona hakuna maambukizi mapya yanayoweza kutokea kwa
kufuatlia na kuchukuwa hatua ikiwemo elimu kwa umma kama walivyokuwa wakifanya
awali.
Nae Meneja wa Kampuni ya uuzaji na uzalishaji wa Pembejeo za
kilimo YARA Kanda ya kaskazini Philipo Mwakipesile alisema kuwa kampuni hiyo
imetoa msaada huo wenye thamani ya million 82 kwa mawakala wa pembejeo wa
ukanda huu wa kaskazini na walianza na Uknda wa kusini na watamalizia ukanda wa
ziwa.
Alisema lengo la utoaji wa vifaa hivyo vya kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu kwa mawakala ni kuunga mkoano
serikali kuhakikisha inaendelea kupunguza maambukizi mapya na kuona ugonjwa huo
unaondoka ndani ya jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla kwa kuwa
umechukuwa nmaelfu ya wenzetu duniani kote hivyo sekta ya kilimo ni muhimili
mkubwa wa uchumi hapa nchini ndio maana wakaona waanze nayo.
No comments:
Post a Comment