KANISA LA ABC LA TABATA JIJINI DAR ES SALAAM KUWEKEZA KWENYE MIRADI KUSAIDIA JAMII - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP

Habari Mpya

.com/img/a/

Tuesday, 10 December 2019

demo-image

KANISA LA ABC LA TABATA JIJINI DAR ES SALAAM KUWEKEZA KWENYE MIRADI KUSAIDIA JAMII

1
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila (kushoto),akiongoza kumuombea Askofu wa Kanisa hilo, Flaston Ndabila na mke wake Janeth katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jana.

_MG_9037
Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo. 

_MG_9052 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiwapungia mikono waumini wa kanisa hilo wakati wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo.

_MG_8983
 Watoto wakiwa katika maadhimisho hayo.

_MG_8992
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_8997
 Watumishi wa Mungu kutoka nje ya nchi wakionesha mshikamano kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Bishop Mark Mugekenyi (Kenya) na Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi .

_MG_8998
 Nyimbo zikiimbwa.

_MG_8999
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_9000
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_9001
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_9012
 Nyimbo zikiimbwa.

_MG_9014
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiingia kanisani.

_MG_9021
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiingia kanisani. Kutoka kushoto  ni  Rehema, Tabitha na kaka yao Gadi.

_MG_9024
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiwa na Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani).

_MG_9074
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_9075
 Maadhimisho yakiendelea.

_MG_9076
 Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church Dkt  David Mwasota, akiomba kabla ya kuanza kwa maadhimisho hayo.

_MG_9094
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, akitoa historia fupi ya kanisa hilo.

_MG_9098
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiwa katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni  Gadi, Rehema na Tabitha.

_MG_9103
 Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Peter Sifi akitoa taarifa ya kanisa hilo.

_MG_9104
 Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), akiomba katika maadhimisho hayo.

_MG_9131
 Bibi na Bwana Dickson Malali wakizungumzia kanisa hilo.

_MG_9136
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakizungumzia kanisa hilo.

_MG_9139
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakikabidhi zawadi.

_MG_9145
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakipokea zawadi ya mashine ya kufulia.

_MG_9146
 Bwana na Bibi, Martin Muhembano wakizungumzia kanisa hilo.

_MG_9155
 Pastor Florian Katunzi  na mke wake Rachel wakizungumza.

_MG_9156
 Bishop Musa Ngobese kutoka Afrika Kusini, akizungumza.

_MG_9159
 Bishop Mark Mugekenyi,  akizungumza.

_MG_9161
 Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, akikabidhi zawadi.

_MG_9162
 Askofu Primus Ishobeza, akikabidhi zawadi.

_MG_9165
Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), akikabidhi zawadi.

_MG_9170
 Zawadi ya vitenge ikienda kutolewa.

_MG_9175
 Majirani wa kanisa hilo wakitoa zawadi ya jogoo.

_MG_9177
 Majirani wa kanisa hilo, wakizungumza.

_MG_9181
 Wanafamilia ya Askofu Ndabila katika picha ya pamoja.

_MG_9184
 Keki ikikatwa.

_MG_9187
 Watoto wakilishwa keki.

_MG_9189
Mchungaji, Nathaniel Ndabila akifunga maadhimisho hayo kwa maombi.

Na Dotto Mwaibale

KANISA la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam linatarajia kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuweza kusaidia jamii hasa vijana waweze kujikomboa kiuchumi.

Hayo yalielezwa jana katika hafla ya  maadhimisho ya miaka 25 ya huduma ya kanisa hilo wakati wa utoaji wa taarifa fupi iliyosomwa na Peter Sifi ambaye ni Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila.

"Katika kipindi hiki cha miaka 25 ya huduma ya kanisa letu tumefanya mengi lakini sasa tunataka kujikita katika uwekezaji wa kujenga chuo cha biblia ambacho ndani yake kutakuwa na chuo cha ufundi " alisema Sifi.

Alisema chuo hicho, kitatoa mafunzo ya ufundi washi, umeme, ushonaji, kompyuta, ujenzi, ushauri wa masuala ya ujasiriamali, useremala  na kuwa  tayari kanisa hilo limetenga sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa kisasa  ambao ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni eneo la Kifuru Manispaa ya Ilala.

Alisema lengo la kuanzisha kwa uwekezaji huo ni kutoa fursa kwa wachungaji watakao kuwa wanasoma kwenye chuo hicho kujifunza stadi za kazi mbalimbali badala ya kutegemea uchungaji pekee na baada ya mafunzo hayo nao wapeleke elimu hiyo kwa jamii.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God  (EAGT) Dkt.Asumwisye Mwaisabila ambaye ni miongoni mwa wazee wenye wanaoheshimiwa aliyedumu katika imani kwa muda mrefu akifanya kazi pamoja na Mzee Moses Kulola na Mungu amemjalia neema katika imani na usemi aliwataka wachungaji kufanya kazi ya utumishi kwa nguvu zote ili waje waweke alama ya utumishi wao.

"Kazi ya utumishi inahitaji uvumilivu na kujituma na sio mchezo mchezo mwenzetu Ndabila sasa anaadhimisha miaka 25 tangu aanze huduma hii na amepita katika magumu mengi na leo anamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapa alipo mungu aendelee kumbariki zaidi huduma yake ikue zaidi ya hapo" alisema Mwaisabila.

Askofu Flaston Ndabila akitoa historia fupi ya kanisa hilo alisema yeye na mke wake walipita katika changamoto nyingi ikiwemo ya kulala njaa wakati wakianza huduma hiyo ya kichungaji huku wakiwa na mshirika mmoja tu kwa kipindi cha miaka miwili. Alisema wanamshukuru mungu kwani hivi sasa wanawachungaji na baadhi ya makanisa yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi alisema Tanzania ni nchi rafiki na nchi ya Burundi kwani ilijihirisha mwaka 2015 wakati lilipotokea jaribio la kutaka kumpindua Rais wa nchi hiyo wakati yupo hapa ambapo Tanzania ilisaidia kumrudisha nyumbani na mapinduzi hayo kushindwa.

Akimzungumzia Askofu Ndabila, Tharcise alisema mafunzo aliyompa yamemsaidia sana katika kanisa lake na yamebadilisha maisha yake ukilinganisha na hapo mwanzo.

Katika maadhimisho hayo maaskofu na wachungaji kutoka ndani na nje ya nchi walihudhuria baadhi yao ni Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, Bishop Mark Mugekenyi (Kenya), Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church Dkt  David Mwasota, Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), Pastor Florian Katunzi na Askofu Primus Ishobeza na wengine.
Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *