VIONGOZI WA DINI KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 28 November 2019

VIONGOZI WA DINI KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

 Viongozi wa dini mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kukutana jijini Mwanza ili kwa pamoja kusaini maazimio ya kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa Kifua Kikuu (TB) kupitia nyumba zao za ibada.

Mwenyekiti wa kambi rasmi ya wabunge wanaopambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, Oscar Mkasa (kuli) ameyasema hayo Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusiana na shughuli hiyo.

Mkasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Madawa ya Kulenya amesema shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika Ijumaa Novemba 29, 2019 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) amebariki shughuli hiyo akisema itasaidia kutoa elimu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao takribani asilimia sita ya wagonjwa wote nchini wanatoka mkoani humo.
Na George Bingai, Mwanza


No comments:

Post a Comment