KIPYENGA CHA KUJAZA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA CHAFUNGWA LEO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 28 November 2019

KIPYENGA CHA KUJAZA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA CHAFUNGWA LEO


Na Ahmed Mahmoud Arusha

MCHAKATO wa uchaguzi mdogo kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Mapiduzi CCM mkoa wa Arusha ambayo hadi sasa inashikiliwa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Lotha Sanare umefungwa leo ambapo zaidi ya wagombea 40 wamejitokeza kuomba nafasi hiyo.

Uchaguzi huo unakuja baada ya Nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na mwenyekiti aliyekuwepo Loatha Sanare kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro mapema mwezi wa kumi mwaka huu.

Mchakato huo ambao ulianza November 25 umevuta hisia za waombaji wa nfasi hiyo ambao wameonyesha hamasa kubwa wakati wa kuchukuwa na kurudisha fomu licha ya uongozi wa mkoa wa chama hicho kutotaja majna hadi sasa.

Licha ya kuwepo uchaguzi huo mdogo hadi wagombea wanarudisha fomu zao za kuomba nafasi hiyo chama hicho kimekuwa kwenye usiri mkubwa tokea siku ya mwanzo ya kutoa fomu hadi leo siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo.

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo mara baada ya kurudisha fomu mmoja ya wagombea wa nafasi hiyo Charles Panga ambaye ndiye mgombea kijana zaidi kati ya waliogombea nafasi hiyo alisema kuwa umri sio tatizo la uongozi bali mawazo ya kiuongozi na utendaji ndio silaha kubwa kwa mwanasiasa.

Alisema kuwa amejipanga pindi atakapopitishwa kwenye uchaguzi huo kuhakikisha chama hicho kinaisimamia serikali kutekeleza ilani ya chama hicho 2020 na kuwa daraja la wananchama wapya kuweza kuongoza kwa vitendo na kuacha siasa za kizamani za makundi ndani ya chama hicho.

“Nitakuwa sehemu ya kukipigania chama changu na wakati wote nitakuwa tayari kupokea maelekezo ya kufikia sehemu ya kuendelea chama change kushika dola na kushinda chaguzi mbalimbali”alisema Panga.

Alisema kuwa chama hicho pindi akipata ridha hiyo atasaidiana na viongozi kuhakikisha kuwa wananchi na wanyonge kero zao zinashughulikiwa kwa kuwa chama ndio mtetezi wa wananchi hao naye kuwa sehemu ya kuwasaidia wananchi kufikia malengo hayo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo au mwishoni mwa wiki ambapo hadi sasa wananchama wa chama hicho wapo mkao wa kula kuhakikisha wanampata mwenyekiti wao wa mkoa katika uchaguzi huo.

Duru za kisiasa mkoani hapa zimejikita kwa wagombea kuhakikisha wanapata mwenyekiti sahihi wa kuvaa viatu vya Loatha Sanare ambaye utendaji wake ulimfanya mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Rais Dkt.John Magufuli kumchagua kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kuchukuwa nafasi ya Dkt. Kabwe Stephen na hivyo kuvutia wagombea zaidi ya 40 hadi dirisha lilipoungwa saa kumi jioni November 27.

No comments:

Post a Comment