KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHAKABIDHI MADARASA MANNE NA VYOO KUMI KWA KUTUO CHA WATOTO WENYE MAHITAHJI MAALUM CHA BUHANGIJA I - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 11 November 2019

KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHAKABIDHI MADARASA MANNE NA VYOO KUMI KWA KUTUO CHA WATOTO WENYE MAHITAHJI MAALUM CHA BUHANGIJA I

Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako  akizindua madarasa manne ya Kituo cha watoto walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi cha wake wa viongozi cha New Melleanium Women Group. Wa nne kulia ni Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda, kulia ni Mama Hasina Kawawa, wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mlezi wa kikundi cha Wake wa Vingozi cha Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na watoto wa kituo cha walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kikundi hicho kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa shule hiyo, Novemba 10, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) na  Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu , Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia) wakiwapa  chakula watoto wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa na vyoo kumi, Novemba 10, 2019.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment