TANZANIA KUNUFAIKANA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIANINFRASTRUCTURE INVESTMENT’ - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 21 October 2019

TANZANIA KUNUFAIKANA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIANINFRASTRUCTURE INVESTMENT’

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’  yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.


Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.

No comments:

Post a Comment