|
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na Daniel Ngwema Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpira wa Kilimahewa kwa ajili ya kushuhudia fainali ya timu ya Nyakahanga dhidi ya timu ya Magambo katika mashindano ya ligi ya Bashungwa Karagwe Cup iliyofanyika katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe.Godfrey Mweruka akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe.Innocent Bashungwa. |
|
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya cheti mshangilia bora wa mashindano ya Ligi ya Bashungwa Karagwe Cup kabla kufunga mashindano hayo. |
|
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na viongozi wa mkoa wa Kagera wakiwa wameshika kombe kwa ajili ya kumkabidhi timu ya Nyakahanga iliyoibuka kidedea katika Mashindano ya Ligi ya Mpira wa miguu ya Bashungwa Karagwe Cup. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).
|
|
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Mweruka akisalimiana na wachezaji wa timu Nyakahanga kabla ya mchuano huo kuanza katika uwanja wa Kilimahewa uliopp katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. |
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amefunga Mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ya Bashungwa Karagwe Cup ambapo timu ya Nyakahanga imeibuka kidedea dhidi ya timu ya Magambo. Akizungumza kabla ya kufunga mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka vijana kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kupitia michezo.
Naye, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe.Innocent Bashungwa ambaye ni Mbunge wa Karagwe na Mratibu wa Mashindano hayo amesema umati wa watu waliojitokeza kushuhudia Mashindano hayo ni ishara tosha ya umoja na mshikamano wa wakazi wa Karagwe kwa Mbunge wao.
No comments:
Post a Comment