SHIRIKA LA TTCL LAZINDUWA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 7 October 2019

SHIRIKA LA TTCL LAZINDUWA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA...!

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akikata keki kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba akishuhudia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (wa pili kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga mara baada ya kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL iliyofanyika katika duka la huduma kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kulia) akimlisha keki mmoja wa wateja wa TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kulia) akizungumza na wateja wa TTCL (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam.

Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam.

Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa  TTCL leo jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA
la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) leo limezinduwa rasmi maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja huku likisisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kuleta mapinduzi makubwa  katika eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu kwenye bidhaa zake.

Akizinduwa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga amesema shirika litaendelea kufanya mapinduzi makubwa  eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu katika bidhaa zake ili kuhimili ushindani uliopo sokoni.

Alisema ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwaka unaoishia Desemba 2018, ilibaini kuwa TTCL ni Shirika la huduma za Mawasiliano linalokua kwa kasi, huku likiongoza kwa idadi ya ongezeko la wateja na hata huduma ya T PESA nayo ikitajwa miongoni mwa huduma zinazostawi kwa kasi kubwa.

"Hadi sasa, tumeweza kuwafikia asilimia 2 ya Wateja wa huduma za simu Nchini , yaani Wateja  zaidi ya milioni mbili  huku huduma ya  T PESA ikifikisha Wateja zaidi ya laki nne, Mawakala elfu kumi na nne  na miamala ya takribani Tsh bilioni tano za Kitanzania."

Aidha alisema katika kuwajali zaidi wateja wake kihuduma TTCL imezinduwa rasmi huduma ya TTCL App na namba maalum ya WhatApp ya Huduma kwa wateja kuboresha zaidi huduma zake.

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba aliongeza kuwa kila mwaka, wamekuwa wakiwapatia wateja wao  huduma mpya na huduma ya mwaka huu itaenda sambamba na utoaji wa zawadi kemkem za kuonesha shukrani kwa wajeja wao.

"Mwaka huu 2019, tunawaletea huduma ya TTCL App ambayo ni Application itakayowawezesha Wateja wa TTCL Corporation kujiunga na vifurushi, kuongeza salio na kupata salio la akaunti yake kupitia simu za mkononi (i.e simu janja) na tablets."

Akifafanua zaida huduma hizo, alisema ndani ya TTCL App mteja ataweza kuongeza na kuangalia salio kupitia App hiyo  itakayopatikana bure kwa wateja wa TTCL bila kujali kama ana kifurushi cha intaneti muda huo.

"Wateja watakaotumia TTCL App wataweza kupata huduma za ziada kama dondoo za afya, soko la hisa na kubadilisha fedha, kuona matangazo mbalimbali ya TTCL, kuunga kifurushi kwa namba nyingine, kumnunulia rafiki muda wa maongezi  nk.

"TTCL App haitaji usajili maalumu ili kutumia. Sisi tumetimiza wajibu wetu, kazi kwenu Wateja wetu, kufurahia huduma hii nzuri na rahisi sana kuitumia. Pamoja na TTCL App, tumewaongezea Wateja wetu njia nyingine rahisi ya kuwasiliana nasi kupitia Huduma ya WhatsApp ambapo kwa namba 0738 151511, alisema.

Huduma zikiendelea kwenye duka la TTCL Samora jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Tupo tayari kuwahudumia wateja wetu kwa bashasha...! Ndivyo wanavyoonekana watoa huduma wa TTCL kwenye maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment