RAIS DK MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 20 October 2019

RAIS DK MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment