MAKATIBU WAKUU WA NCHI 16 WAKUTANA ARUSHA KUWEKA AGENDA YA MKUTANO WA SADC KWA MAWAZIRI WA SEKTA ZA MAZINGIRA,MALISILI NA UTALII - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 21 October 2019

MAKATIBU WAKUU WA NCHI 16 WAKUTANA ARUSHA KUWEKA AGENDA YA MKUTANO WA SADC KWA MAWAZIRI WA SEKTA ZA MAZINGIRA,MALISILI NA UTALII

Katibu Mkuu wa Wizara ya Malisili na Utalii ,Prof ,Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu wakuu na Maafisa Waandamizi wa Sekta za Mazingira ,Malisili na Utalii kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo, kusini mwa Afrika (SADC).
 
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .

Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa  Sekretarieti ya SADC ,Domingos Gove akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoshirikisha Makatibu Wakuu kutoka nchi 16 za SADC.

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .

Baadhi ya Makatibu Wakuu wanaoshiriki Mkutano huo. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,prof ,Adolf Mkenda akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.

Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa Sekretarieti ya SADC,Domingos Gove akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC. 

  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira ,Joseph Malongo akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.

Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi  wa Sekta ya Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC ,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika kituo cha kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini Arusha.

Na Dixon Busagaga, Arusha

MAKATIBU wakuu wa Sekta na Maafisa waandamizi wa Wizara zinazo shughulika na Mazingira, Maliasili na Utalii wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kuweka agenda za Mkutano wa Mawaziri wa sekta husika kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).

Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kikao hicho cha awali ni pamoja na mpango mkakati wa pamoja wa kukabiliana na ujangili kwa nchi za SADC, hoja inayo paswa kuungwa mkono nan chi wanachama.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda amesema  nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.

“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC, hii ni moja kati ya agenda muhimu zitakazojadiliwa,” alisema Profesa Mkenda.

Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili kutoka Sekretarieti ya SADC, Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya Mazingira, Utalii na Wanyamapori.

Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo amesema kuwa watajadili mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa pamoja na jinsi ambavyo wananchi wanaweza kutumia uchumi wa bluu kwa maana ya bahari katika kuchangia maendeleo.

No comments:

Post a Comment