NA KHALFAN SAID
WANAHISA
zaidi ya 400 wa Mwalimu Commercial Bank
Plc (MCB) wamekutana mjini Mtwara katika mkutano wa mwaka (AGM) na kupokea
taarifa ya kiutendaji ya benki hiyo kwa mwaka 2018.
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa amesema Mkutano huo
wa tatu ni wa kawaida ambao lengo lake ni kuwapa taarifa ya kiutendaji ya benki
ambapo wanahisa wataijadili na kuweka maazimio mbalimbali ya kiutekelezaji kwa
wakati ujao.
“Sisi
kama taasisi ya kifedha, kila mwaka huwa tunafanya mkutano wa wanahisa ili
kuwaeleza hali ya benki yao, Shughuli zilizofanyika kwa mwaka mzima, mafanikio
yaliyopatikana, changamoto na matarajio ya baadaye, lakini pia kupokea maoni
kutoka kwa wanahisa wetu ambao pia ni wateja wetu wanayo nafasi kubwa sana ya
kutoa maoni yao kwa nia ya kuboresha uendeshaji wa benki.” Alifafania Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Makungwa.
Alisema
wengi wa Wanahisa wa Mwalimu Commercial
Bank Plc ni walimu lakini pia wako wanahisa ambao sio walimu, kuna
mashirika na taasisi nyingine kwani benki hii ipo kuhudumia Watanzania wote.
Mwalimu
Commercial Bank Plc kama zilivyo benki nyingine za biashara
inafanya shughuli zote za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wateja wake.
“Benki
yetu inatoa mikopo ya binafsi, mikopo ya biashara zikiwemo biashara ndogo ndogo
na kwakweli tumekuwa na mafanikio makubwa, wateja wetu ni waaminifu wanarejesha
mikopo waliyopewa pamoja na changamoto za hapa na pale lakini bado tunafanya
vizuri katika eneo hilo.” Aibainisha.
Alisema
licha ya benki kutumia mifumo yake ya kawaida katika kutoa huduma lakini pia
inakusudia kuendeshwa kidigitali ili mteja popote alipo aweze kufanya miamala
bila shida yoyote na hivi karibuni benki itajiunga na mtandao wa VISA ambao utawawezesha
wateja wetu kupata huduma za kibenki mahala popote walipo.
“Benki
inaendelea kuboresha huduma zake, wanahisa na wateja wetu wategemee kuwa benki yao inaendelea kuboresha
huduma zake na kuimarika walimu wetu ambao ndio wateja wetu wakubwa wako nchi
nzima na tunajitahidi kuhakikisha huduma zetu zinawafikia kwa urasihi.”
Alifafanua.
Alitoa
hakikisho kuwa Mwalimu Commercial Bank
Plc iko katika hali nzuri na mtaji wake uko vizuri na unakidhi matakwa ya
msimamizi wa mabenki yaani BoT.” Alisema.
Akifungua
Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Herman Kessy alisema, benki imepata leseni
ya uwakala wa bima na hivyo itawaomba wadau Chama cha Walimu (CWT), Mfuko wa
Pensehni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
kutumia huduma hiyo kwa faida ya benki na wanahisa wote.
Pia
Bw. Kessy alisema katika mafanikio ya benki kwa mwaka 2018 ni pamoja na
kuongeza tawi la pili pale Mlimani city, lakini kufungua ofisi kwa ajili ya
kutoa huduma kwenye mikoa ya Morogoro na Mwanza na Mbeya.
Awali
wajumbe wa mkutano huo walipatiwa semina iliyoendeshwa na Meneja wa Huduma za
kidijitali Bw. John Mhina iliyolenga kuwaelimisha nidhamu ya matumizi ya fedha
na umuhimu wa kuweka akiba.
Wajumbe
pia walipata elimu kuhusu soko la hisa umuhimu wa walimu kununua hati fungani
ambapo Mkuu wa Uendeshaji na Fedha wa kampuni ya Core Security Limited ambayo ni wakala wa soko la hisa la Dar es
Salaam,Bi. Mary Kessy alifafanua kuhusu namna ambavyo mtu anaweza kununua hati
fungani.
Bw. Kessy akihutubia wajumbe.
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw. Richard L. Makungwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
Wanahisa wakipitia taarifa mbalimbali kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
Mwanahisa akipitia taarifa hiyo ya utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
Baadhi ya wajumbe wa bodi wakiwa pamoja na wanahisa wa benki hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi.
Wajumbe wa bodi Profesa Tadeo Satta (kulia) na Bw. Framncis Ramadhani wakizungumza jambo.
Mwanasheria wa benki akitoa ufafanuazi wa masuala mbalimbali yahusuyo mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Deus Seif (aliyesimama), akizunguzma kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja wajumbe wa bodi na baadhi ya viongozi wa chama cha walimu CWT.
No comments:
Post a Comment