Jenister Mhagama, Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. |
OFISI ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni, 2019.
Maadhimisho haya husherehekewa kila mwaka na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuonesha mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya Nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.
Katika maadhimisho hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inawakaribisha wadau wake na wananchi wote kuja kupata huduma katika ofisi zake zilizopo katika Mji wa Serikali, Kata ya Mtumba na zilizopo ghorafa la PSSSF Mtaa wa Makole.
Mnakaribishwa kuleta maoni na ushauri ili kupata ufumbuzi wa pamoja na kuleta ufanisi katika sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu. Huduma zitatolewa kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 9:30 Alasiri.
NYOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
No comments:
Post a Comment