Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw (kushoto) akizungumza na wanahisa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka 2019 (AGM), uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mkutano Mkuu wa Mwaka 2019 wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wanahisa wa Benki ya NMB wakijisajili kabla ya kuanza kwa mkutano wao mkuu. |
WANAHISA wa Benki ya
NMB wameidhinisha kiasi kilichopendekezwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka
(AGM), uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ikiwa ni matokeo ya
utendaji bora na uimara wa nafasi ya mitaji, malipo ya jumla ya gawio la
Shilingi Bilioni 33 (sawa na Shilingi 66 kwa kila hisa), yanafanana na sera ya
benki ya kulipa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya faida la jumla baada ya makato
ya kodi (PAT) katika gawio. Hiliniongezeko la asilimia 3 ukilinganisha na bei
ya Shilingi 64 kwa kila hisa iliyolipwa mwaka uliopita. Nia ni kukuza kiwango
cha gawio kwa kila hisa, kulingana na utendaji bora wa benki unavyoongezeka.
Benki iliripoti faida
ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 142 kabla ya makato ya kodi (PBT), kwamwaaka
wa fedha ulioishiaDesemba 31 2018; ambayo ni ongezeko la asilimia 3 kutoka
faida ya Shilingi Bilioni 138 iliyopatikana mwaka uliotangulia. Licha ya mafanikio
yaliyopatikana, Bodi na Uongozi wa Benki ya NMB umeridhishwa na aina ya
mafanikio na mapinduzi chanya katika kipindi cha mwaka.
Mapinduzi hayo ni
pamoja na uzinduzi wa NMB KLiK, mikopo ya mshahara - ambayo ni bidhaa ya
kwanza ya benki kutoa mkopo kwa njia ya simu. Kuanzishwakwa Mawakala zaidi ya
6800, wanaoshughulika – pamoja na mambo mengine, ukusanyaji na ulipaji wa kodi,
ushuru na mapato ya Serikali za Mitaa katika Halmashauri 180, mapinduzi
yanayochangiamzunguko wa pesa kwa mifumo ya kidijitali na kukuza amana. Pia
tumeimarisha huduma za kibenki kupitia mtandao ilikuhudumiavizuri zaidi akaunti
za makampuni na kuwapa suluhisho zote
kamilifu na kufanya miamala ambayo imesababishaongezeko la wateja kutoka
milioni 2.2 hadi milioni 3.1 mwishoni wa mwaka 2018 .
UimarawaNMB kama taasisi
za fedhaimepelekea Moody kuipaalama ya B1 ambayo vimethibitishakuaminiwa kwa
Benki ya NMB na wawekezaji wa kimataaifa. Benki imeimarishwavemanauwiano wa
mtajikwa asilimia 16.5. Hiyo inamaanisha kwamba benki yetu ikosalama kabisa
kibiashara Mwenyekiti wa Benki, Prof.
Joseph Semboja, anabainisha kuwa Bodi inataka kuweka sawaongezeko la
wanahisa, sambamba na kuimarisha biashara ya fedha ndani ya benki katika mpango
mkakati wa kukua zaidi kiuchumi.
“Kwa miaka kadhaa sasa
NMB imeendelea kuwa imara yenye afya kifedha, lengo ni kuendelea kuimarika
zaidi na kubaki hivyo. Ili kufikia mafanikio haya, tunapaswa kuhakikisha
tunafanyamaamuzi sahihi hasa katika udhibiti wa mabadiliko kwenye mahitaji
makuu ya kimtaji,” anasema Mwenyekiti.
“NMB imejipambanua
katika kuendelea kusaidia harakati za maendeleo ya uchumi Tanzania nakuvuka
kiwango cha sasa cha dira ya uchumi kama kichocheo cha ujenzi wa miundombinu ya
kiuchumi nchini. Tutaendelea kuwa vinara wa hudumaa bora kwa wateja wetu, huku
tukiendelea kutimizawajibu wetu kwa jamii,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw.
NMB imejitolea katika
kusaidia ukuaji kiuchumi wa wajasiriamali wadogo na
wakati (SME's), hususani wanawake kwa kuwapa mafunzo na elimu ya uwezeshaji
katika kuimarisha biashara zao kwa kutambulishajukwaa jipya la ‘Woman in
Banking’ kote nchini. Katika kilimo, NMB tumeboreshajopo la
wataalamuwanaojikita zaidi katika Sekta ya KilimoBiashara,
ilikuimarishamnyororo wa thamani unaopewausaidizi mkubwa na Taasisi ya NMB
Foundation, ambayo inatoa elimu katika Taasisi za Sekta ya Kilimo.
"Sisi ni Benki
Bora Tanzania. Ubora wetu ni katika nyanja zote, za utawala, teknolojia ya
habari na mfumo mzima unaoifanya NMB kuwa benki salama nchini, huku tukihakikisha
amana na akibazakozikosalama chini yetu," aliongeza.
No comments:
Post a Comment