WAZIRI MKUU AWASHAURI WATANZANIA KUJIWEKEA AKIBA KUPITIA HISA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 17 June 2019

WAZIRI MKUU AWASHAURI WATANZANIA KUJIWEKEA AKIBA KUPITIA HISA

Waziri Mkuu Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa Timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kikombe cha ushindi wa mechi ya soka  ya kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya Bunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akimtoka mlinzi wa timu ya Soka ya Bunge, Rajab Kapira katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma June 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya benki ya CRDB wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi  baada ya kuitandika timu ya Bunge 3-1 katika mechi ya kirafiki ilichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete akijiandaa kurusha mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya Mpira wa Pete ya Bunge na timu ya Benki ya CRDB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kuanza kujiwekea akiba kwa kununua hisa kupitia taasisi za kifedha nchini ikiwemo benki ya CRDB. Ametoa kauli hiyo Juni 16, 2019 wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya CRDB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema suala la wananchi kujiwekea akiba ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yao. "Nashauri wananchi tutumie taasisi za fedha kujiwekea akiba pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya maendeleo yetu."

Akizungumzia kuhusu bonanza hilo lililoandaliwa na benki ya CRDB, Waziri Mkuu amesema michezo ni sehemu nzuri kujenga afya, furaha na kujenga mshikamano wa karibu baina ya benki hiyo na wananchi ambao ni wateja.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya CRDB ilishinda baada ya kuifunga timu ya Bunge penati tatu kwa moja na kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuibugiza CRDB magoli 35 kwa mawili.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za CRDB. Upande wa mchezo wa basketball timu ya Bunge ilishinda vikapu 53 kwa 51.

No comments:

Post a Comment