RAIS DK MAGUFULI AMETOA MKONO WA POLE KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR KWA KUFIWA NA MKE WAKE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 23 June 2019

RAIS DK MAGUFULI AMETOA MKONO WA POLE KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR KWA KUFIWA NA MKE WAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) Mikocheni jijini Dar es salaam ambaye amefiwa na mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiomba dua maalumu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) pamoja na familia yake nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es salaam kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar(Mke wa Naibu katibu mkuu CCM Znz) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu wa Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Znz Balozi Sefu Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi  na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi wakimuombea dua marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment