MAAFISA WA TANAPA WAVIKWA VYEO VYA KIJESHI...! - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Sunday, 23 June 2019

demo-image

MAAFISA WA TANAPA WAVIKWA VYEO VYA KIJESHI...!

IMG_0413 Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dk. Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwavisha vyeo vinavyoendana na mfumo wa Jeshi'Usu katika uendeshaji wa Shirika hilo kwa Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 na Maafisa Uhifadhi Waandamizi 80.

IMG_0390 Baadhi ya Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi  wakiwa katika hafla hiyo.

IMG_0399 Naibu Kamishna Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara,William Mwakilema akizungumza wakati wa hafla ya kuwavisha vyeo vipya Maafisa Wakuu wa Uhifadhi na Maafisa Uhifadhi Waandamizi,hafla iliyofanyika eneo la Mto wa Mbu .

IMG_0392 Baadhi ya Maafisa Uhifadhi Wakuu .

IMG_9994
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano -TANAPA,Pascal Shelutete akitoa maelezo namna ambavyo zoezi la uvikwaji wa vyeo vipya kwa Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi pamoja na Kiapo cha Utii .

IMG_9948
IMG_9951
IMG_9954
 Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi'Usu la Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakila kiapo wakati wa hafla fupi ya kuwavisha vyeo vipya vya nafasi hizo ,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mto wa Mbu -Karatu mkoani Manyara.

IMG_0355
IMG_0357
IMG_0380
IMG_0364 Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwavisha vyeo Maafisa Uhifadhi Wakuu wa Jeshi Usu -TANAPA,wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya Msingi Mto wa Mbu  wilayani Monduli .Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 walivishwa vyeo vipya.

IMG_0306
IMG_0272
IMG_0240
IMG_0248
IMG_0349
IMG_0291
IMG_0218 Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt, Allan Kijazi akiwavisha vyeo Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi'Usu -TANAPA,wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya Msingi Mto wa Mbu  wilayani Monduli .Maafisa Uhifadhi Waandamizi  80 walivishwa vyeo vipya .
IMG_0437
IMG_0462 Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt ,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Maafisa Uhifadhi Wakuu wa Jeshi Usu -TANAPA,mara baada ya kula kiapo na kuvishwa vyeo vipya .Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 walivishwa vyeo vipya . 

IMG_0465
Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi Usu - TANAPA, mara baada ya kula kiapo na kuvishwa vyeo vipya. Maafisa Uhifadhi Waaandamizi 80 walivishwa vyeo vipya.

Na Dixon Busagaga

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) (CC), Dk. Allan Kijazi amewavisha vyeo vipya Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi, vyeo vinavyoendana na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa shirika hilo kutoka ule wa kiraia na kuwa Jeshi Usu.

Zoezi la uvishwaji vyeo kwa Maafisa hao 99 wa vitengo mbalimbali katika shirika hilo limefanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mto wa Mbu, wilayani Karatu na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya.

Akizungumza mara baada ya Maafisa hao kula kiapo cha Utii, Kamishna wa Uhifadhi –TANAPA, (CC) Dk. Kijazi aliwataka kuhakikisha suala la ulinzi na usalama wa Hifadhi unaimarika zaidi pamoja na kushirikiana na wananchi katika kulinda rasilimali za taifa .

“Ni wakati wa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ujangili na hii ni kutokana na kasi ya matukio ya ujangili kuongezeka katika baadhi ya hifadhi”alisema Dk. Kijazi .

Vyeo vipya vimetolewa wa Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 na Maafisa Waandamizi 80 ikiwa chachu ya kuendelea na majukumu yao wakiwa katika mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi Usu.
Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *