MEYA WA JIJI LA DAR MWITA AKUTANA NA MEYA WA ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 15 June 2019

MEYA WA JIJI LA DAR MWITA AKUTANA NA MEYA WA ZANZIBAR

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Khatibu A Khatibu.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Khatibu A Khatibu ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kuhusiana na namna ya uendeshaji wa majiji.
Aidha mameya hao wawili kwa pamoja wamebadilishana uzoefu wakuendesha majiji hayo hususani katika suala la ukusanyaji wa mapato, kutangaza utalii ikiwa ndio sehemu kubwa ya upatikanaji wa mapato.
Meya Mwita amesema kuwa ujio huo ni mahususi kwa wananchi kutambua kwamba viongozi waliochaguliwa wanashirikiana vizuri katika kuwaletea maendeleo.
Aidha Meya Mwita amemshauri  Meya wa Zanzibar Khatibu, kwamba katika kuleta maendeleo jijini humo, anapaswa kushirikiana vizuri na wananchi, madiwani bila kujali itikadi za vyama vyao kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha kuleta maendeleo makubwa.
Mbali na hivyo pia amemshauri kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya utalii kwakuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato na kwamba Zanzibar ndio kitovu kikubwa cha utalii Tanzania Visiwani.
 Kwaupande wake Meya Khatibu amemshukuru Meya Mwita kwamapokezi mazuri nakusema kuwa amejifunza uzoefu mkubwa kupitia kwakwe na kwamba ziara hiyo itamsaidia kuendesha jiji la Zanzibar.
Amesema kuwa awali Zanzibar haikuwa kama jiji, lakini kuanzia Julai mosi mwaka huu litatambulika na kwamba kwanafasi yake ataliwezesha jiji hilo kufika mbali ikiwa ni pamoja na kufahamika kimataifa.
Ameongeza kuwa ujio huo umetokana na sheria iliyounda  jiji la Zanzibar inatokana na jiji la Dar es Salaam na hivyo hana budi kuja kuchukua uzoefu na mikakati ambayo inatumika kuendesha jiji hilo.
Amesema ushauri aliopewa na Meya Mwita ameupokea na kwamba itakuwa kama dira ya kumuongoza katika utendaji wake hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee kwakuwa wote wanawatumikia wananchi.

No comments:

Post a Comment