|
Askari Mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga akimwekea kwenye mikono Dawa ya kusafishia mikono msafiri aliyekuwa akipita katika mpaka huo wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13, Juni 2019. |
|
Daktari katika mpaka wa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, Anna Anthony, akiwapima wasafiri wanaopita katika mpaka huo, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. |
|
Baadhi ya Wataalamu wa Afya wakimhudumia mmoja wa wasafiri waliokuwa wakipita katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza kuugua, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. |
|
Mtaalamu wa Afya akinyunyizia dawa gari ambalo lilikuwa limewabeba abiria walioigiza kuumwa wakati wakitaka kupita katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. |
KUFUATIA zoezi linaloendelea mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linajikita katikaKupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, tarehe 13 Juni, 2019, Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzania na Kenya, katika makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika Kupima kwa vitendo hatua za kujiandaa na kukabili Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa.
Wataalam hao wameweza kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza madhara ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Wanyama na Binadamu.
Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu.
No comments:
Post a Comment