RAIS WA KONGO (DRC) MHE. FELIX TSHISEKEDI AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE DKT. MAGUFULI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 14 June 2019

RAIS WA KONGO (DRC) MHE. FELIX TSHISEKEDI AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE DKT. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wakiwapungia mikono wananchin waliojitokeza katika sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akikabidhiwa Ua la ishara ya Upendo na kumkaribisha Nchini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Pombe Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli akizungmza na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli.

No comments:

Post a Comment