Hayo yalisemwa na Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Waziri Mohamed (Pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa mwezi wa ramadhani.
Alisema
kuwa mwezi wa ramadhani ni kipindi ambacho waumini humrudia Mwenyezi Mungu kwa
nguvu zote hivyo sio kipindi cha wafanyabiashara hao kujinufaisha kwa watu
wanaofunga kwani waumini wamekuwa wakijidunduliza ili kusaidia
wasiojiweza lakini
wafanyabiashara hao wanaona ni fursa ya kujinufaisha.
“Hiki
ni kipindi ambacho wanawasaidia watu mbalimbali kwa nguvu zao zote, sasa
akamsaidie mtu mwingine na wakati huo huo akusaidie wewe ambaye unataka
kujinufaisha kwa manufaa yako mwenyewe ukijua kabisa kwamba hiki ni kipindi
maalum cha kumrudia Mwenyezi Mungu lakini pia ndugu zangu kwenye tuongeze
ibada,tupendane ikiwemo kutembelea wagonjwa," Alisema.
Katibu
huyo aliwasihi wafanyabiashara kuacha kuongeza bei bei ya vyakula
mbalimbali huku
akiwaomba ikiwezekana washushe bei za vyakula ili kuweza kupata thawabu kwenye
kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtufuku wa ramadhani.
Aidha
aliwatakia mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani Waislamu wote Tanzania pamoja na
wale waumini wa dini mbalimbali watakaosindikiza mwezi huo na kumuomba mwenyezi
Mungu atupe baraka kutokana na mwezi huo ndani ya Mkoa wa Tanga na Tanzania kwa
ujumla.
Hata
hivyo pia aliwataka makatibu wote wa hamasa na chipukizi wilaya za mkoa huo
kuendelela kushikamana ikiwemo kuchangamkia fursa za kimaendeleo zilizopo
kwenye maeneo yao ili ziweze kuwa na tija kwao na jamii
zinazowazunguka.
No comments:
Post a Comment