RAIS DK MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA AFYA MBONDE MASASI, NA BARABARA YA MANGAKA-NAKAPANYA-TUNDURU KM 137 NA BARABARA YA MANGAKA –MTAMBASWALA KM 65.5 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 April 2019

RAIS DK MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA AFYA MBONDE MASASI, NA BARABARA YA MANGAKA-NAKAPANYA-TUNDURU KM 137 NA BARABARA YA MANGAKA –MTAMBASWALA KM 65.5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua moja ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua Masasi mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua chumba cha upasuaji katika wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde Masasi mkoani Mtwara. 

Sehemu ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Masasi mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara akiangalia mashine ya kutoa dawa ya usingizi kkwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji kwa wa mama wajawazito.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza wadau wa Maendeleo, Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kufungua barabara ya Mangaka-Nakapanya-Tunduru km 137 pamoja na Barabara ya Mangaka-Mtambaswala km 65.5 katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto watatu kutoka kushoto aliyeshika utepe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru wasita kutoka kulia aliyeshika utepe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, Wabunge, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Mangaka-Nakapanya-Tunduru km 137 pamoja na Barabara ya Mangaka-Mtambaswala km 65.5 sherehe zilizofanyikka katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikangaula iliyopo Nanyumbu mkoani Mtwara wakati akielekea Mangaka kwenda kufungua barabara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nanyumbu mara baada ya kuwasili kutoka Masasi kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala yenye jumla ya km202.5.PICHA ZOTE NA IKULU.

Sehemu ya wakazi wa Masasi wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia mara baada ya kufungua kituo cha afya cha Mbonde.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungua mkono wananchi hawaonekani pichani wakati akiondoka eneo la kituo cha Afya cha Mbonde.

No comments:

Post a Comment