BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa flana 250 kwa ajili ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza Tanzania ambao wanaenda Zanzibar kushiriki kongamano la michezo.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Afisa Mkuu Mkaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori alisema ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwa Jeshi la Magereza kibiashara kama wateja wao unawasukuma kushirikiana kila linapotokea jambo linaloitaji kushirikiana.
Aliwashukuru Jeshi la Magereza kwa kuwaamini na kuendelea kufanya kazi pamoja na kuwaomba kudumisha ushirikiano huo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Jeshi la Magereza, akipokea msaada huo, Kamishna Msaaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Bertha Mende alisema wanafarijika kuona mara zote wanapoitaji ushirikiano na NMB wanawaunga mkono hivyo kuwahakikishia wataendelea kudumisha. Alisema NMB imekuwa ikiwasaindia mambo mengi bila kuchoka na kuwaomba waendeleze uhusiano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya hafla ya makabidhiano kwa pande zote mbili. |
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa NMB wakishuhudia tukio hilo. |
No comments:
Post a Comment