Washtakiwa wa Mauaji ya kukusudia, Mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Scholasica, Hamis Chacha (aliyebeba maji) , Mwalimu wa Nidhmu katika Shule ya Scholastica, Laban Nabiswa (mwenye shati nyeupe) na nyuma yao ni mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo, mshtakiwa wa pili katika shauri hilo.
Mshitakiwa wa Pili katika shauri la mauji ya kukusudia, Edward Shayo anayetajwa kama mmiliki wa shule ya sekondari ya Scholastica aliyokuwa akisoma Marehemu Humphrey Shayo akiingia katika chumba cha Mahakama.
Na Dixon Busagaga wa
SHAHIDI Irene Mushi
(35) ambaye ni wa kwanza kwenye kesi
ndani ya kesi ya Msingi ya Mauaji ya kukusudia namba CC 48/2018 ya Mwanafunzi
Humphrey Makundi amewasilisha Nyaraka ya Maelezo ya Ungamo ya Mshitakiwa wa
kwanza katika shauri hilo, Hamis Chacha alivyo
tekeleza agizo la Mshtakiwa wa pili, Edward Shayo la kwenda kutupa Mtoni mwili
wa mtu aliyeuawa.
Hatua ya Mahakama kujielekeza katika usikilizwaji wa kesi
ndani ya kesi unatokana na mabishano ya kisheria baina ya upande wa utetezi dhidi ya upande wa
Jamhuri baada ya Upande wa utetezi kuwasilisha hoja ya kupinga kupokelewa kwa
maelezo ya Ungamo katika kesi ya Msingi.
Maelezo ya Ungamo ya Mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo
Hamis Chacha Wisare yalitolewa mbele ya Shahidi wa 14 katika kesi ya Mauaji ya
kukusudia, Irene Mushi, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Moshi mjini ambaye pia
ni mlinzi wa Amani .
Shauri hili linaloendelea Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, mbele
ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na uhujumu Uchumi, Dar es
Salaam, Firmin Maatogoro linawakabili washtakiwa watatu ambao ni Hamisi Chacha, mlinzi wa shule ya Sekondari ya Scholastica, Edward Shayo, mmiliki wa shule na
Laban Nabiswa, Mwalimu wa nidhamu shule ya sekondari ya Schoalastica.
Akiwasilisha kusudio la upande wa utetezi ,Wakili wa
kujitegemea ,Gwakisa Sambo aliieleza
mahakama kuwa upande wa utetezi unapinga maelezo ya mtuhumiwa na kwamba yalichukuliwa bila ridhaa yake ndipo
Mahakama ikajielekeza katika
usikilizwaji wa kesi ndani ya kesi.
Akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali,Joseph Pande,shahidi
Irene Mushi aliieleza Mahakama akiwa na Jukumu la Mlinzi wa Amani alipokea taarifa
kutoka kwa Mfawidhi, akimueleza kwamba kuna mshtakiwa anapelekwa mbele yake kwa
ajili ya kuandika maelezo ya Ungamo.
Alieleza kuwa alifuata taratubu zote na uchukuaji maelezo ya
Mtuhumiwa ikiwa ni pamoja kujibu maswali tofauti ikiwemo kwa nini yupo mbele ya
mlinzi wa amani na endapo maelezo atakayotoa yataenda kutumika kama sehemu ya
ushahidi endapo atafikishwa Mahakamani huku majibu yake yakiwa anafahamu.
Alieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa katika Afya nzuri na kwamba
aliimuliza endapo kama alipigwa ama kutishiwa alimjibu alipigwa tarehe
17/11/2017 na askari Polisi baada ya maelezo yake kutofautiana na ya mlinzi
mwenzake.
Baada ya maelezo hayo Wakili Mkuu wa Seriali, Joseph Pande
alimuonesha karatasi ya maelezo ya mshtakiwa na kuuliza kama anaitambua alijibu
ndio na kuiomba mahakama kuitumia kama kielelezo katika ushahidi wake na
kupokelewa baada ya kuridhiwa na pande zote mbili.
Baada ya kielelezo hicho kupokelewa Shahidi Irene akiongozwa
na Wakili Mkuu wa Serikali anaye wakilisha upande wa Jamhuri katika Shauri hilo
alielekezwa kusoma maelezo yaliyoandikwa katika nyaraka ya maelezo ya ungamo
katika mahakama ya mwanzo Moshi mjini.
Katika sehemu ya maelezo ya Shahidi huyo wakati akisoma
maelezo ya Ungamo ya Mshtakiwa Hamisi Chacha, alieleza kwamba Chacha akiwa eneo lake la kazi alisikia
kishindo cha mtu ndipo alipoamua kupiga tochi na kufuatilia baada ya kubaini
kuwa kuna mtu.
Ameileza mahakama kuwa mtuhumiwa alimueleza kuwa alimpiga mtu
huyo na bapa la Panga na akaumia kenye paji la uso na baadae akampiga bapa la pili na mtu alifariki pale pale ndipo alipompigia simu Mwalimu Laban aliyefika
eneo hilo na kusema huenda mtu huyo amezirai.
Alieleza Labani aliiuliza kama ameshafanya mawasiliano na
Mzee Shayo na baadae alipigiwa Shayo
ambaye anatajwa kama mmiliki wa shule hiyo aliyefika eneo la tukio na kutoa
maelekezo ya mtu huyo kwenda kutupwa mtoni kama hafahamiki na kwamba huenda ni
Kibaka.
Irene ameeleza baada ya hapo yeye Chacha na Mwalimu Labani wakauchukua ule mwili wa marehemu
wakaenda kuutupa mtoni na kurudi shuleni na kuitisha Row call kwa ajili ya kujua
endapo kama ni mwanafunzi hayupo shuleni.
Shahidi alieleza
Mlinzi Chacha alielekea kwenye Mabweni na kukuta kitanda kimoja hakina mwanafunzi na Mwalimu Laban aliuliza ni mwanafunzi gani hayupo, baade ilibainika kuwa mwanafunzi Humphrey Makundi wa kidato cha pili ndio
hayupo.
Upande wa Jamhuri unaaongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Joseph Pande, Wakili wa serikali Mwandamizi, Abdalah Chavula, Wakili wa Serikali, Omari Kibwana na Wakili wa serikali, Lucy Kiusa waliieleza mahakama
kuwasilisha mashahidi wa nne.
Upande wa utetezi
ukiongozwa na Wakili wa kujitegemea, Elikunda Kipoko anaye mtetea
Mshtakiwa wa pili, Edward Shayo akisaidiana na Wakili wa kujitegemea Gwakisa
Sambo, Wakili wa kujitegemea David Shilatu anaye mtetea Mshitakiwa wa kwanza Hamis Chacha na Wakili wa kujitegemea Patrick Paul walieleza mahakama
watawaasilisha shahidi mmoja ambaye ni Hamisi Chacha.
No comments:
Post a Comment