MBIO ZA 'CHIEF MKWAWA' ZAJA,WASHIRIKI WAKARIBISHWA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 18 April 2019

MBIO ZA 'CHIEF MKWAWA' ZAJA,WASHIRIKI WAKARIBISHWA...!

Mkurugenzi wa Mkwawa trail run, Amani Mkwawa akiwa na 
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Lyata pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Hamid Njovu wakiongea na waandishi wa habari juu ya mashindano ya mbio za Mkwawa jinsi gani zitakavyo fanyika.

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa walioshiriki mkutano wa kutangaza kwa kuanza kwa mashindano ya Mkwawa Trail Run.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA
 
MASHINDANO ya Mbio za Mkwawa Trail run yanatarajiwa kufanyika Iringa Juni 16 mwaka huu kwa lengo la kutangaza utalii wa Nyanda za juu Kusini.

Akizungumza na mwandishi waa habari hizi, Mkurugenzi wa Mkwawa trail run, Amani Mkwawa amesema wanariadha watakaoshiriki mbio hizo watakimbia katika mazingira ya mabonde milima na kuvuka mito huku washiriki wakipata historia ya eneo katika kila kituo.
“Mbio hizi ni tofauti na mbio nyingine, hizi zitapita katika maeneo yote yaliyotumika na Chief Mkwawa wakati wa mapambano dhidi ya Ujerumani huku zikirindima kupitia kwenye mabonde, milima, na vivutio vya kihistoria,” alisema Mkwawa.
Mkwawa alisema kuwa mashindano yatafanyika mkoani hapo kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji biashara na vivutio vya kitalii vilivyopo Iringa na nyanda za juu kusini.
Kutunza mazingira na kuendelea kukumbuka na kusherekea maisha ya mashujaa wetu mbalimbali waliotangulia katika kupigania taifa.
Mkwawa alisema kutakuwa na zawadi mbalimbali katika kumbukumbu hiyo kama medali, vyeti na fedha taslimu kwa washindi watatu wa mwanzo.
Kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata aliwaomba wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya Iringa kushiriki katika mbio hizo ili kukuza utalii wa nyanda za juu kusini.
“Hizi mbio zitasaidia kukuza uchumi wetu kwa kutangaza vivutio vilivyopo hapa mkoani Iringa ambavyo hapo baadae tutapa watalii wengi ambao watatuongezea kukuza uchumi wetu” alisema Lyata
Lyata aliongeza kwa kusema kuwa mashindano haya yanasaidia kuendelea kumkumbuka shujaa wa mkoa wa Iringa marehemu chief Mkwawa na wananchi kujifunza namna chief huyo analivyokuwa mchapa kazi.
“Nitoe rai tu kwa mwananchi yeyeto yule ambaye yupo tayari kushiriki mashindano haya anakaribishwa kwa kuwa kila kitu kinaendelea vizuri na niwakaribishe kuweka historia kwenye mbio hizi” alisema Lyata
Naye Naibu Katibu mkuu wa Iringa Tourism Association, Serafino Lanzi amesema washiriki wa mbio hizo watakimbia katika njia ambazo Chifu Mkwawa alipita na kuacha historia ya Mji wa Iringa.
“Mkwawa Trail Run imeandaa njia kufuatana na historia ya maeneo hayo na mbio zitaanzia Uwanja wa Mashujaa Kalenga ulitumiwa na Mkwawa watapita njia ya Mkoga kutokea Kipongoma ambapo ni chimbukizi la mama yake Mkwawa na kupata historia.” Lanzi
Lanzi alisema kuwa washiriki wa mbio hizo watapita Nzihi kurudi Kalenga njia ile alipita mama yake Mkwawa wakati anaenda kutupa dawa zake pale pia tutapita kwenye njia ambayo alitokea Chifu Mkwawa baada ya Wajerumani kupiga ngome wakati anaondoka kwenye ile njia anatokea na mahali hapo ndipo alimuua Mjerumani aliyetaka kumpiga picha Mkwawa.

No comments:

Post a Comment