Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu (katikati). |
Na Mwandishi Wetu, Mihambwe
AFISA Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu ametoa siku mbili kichaka cha majani kilichoota kuzunguka mradi wa Zahanati jirani na makazi ya Watu ufyekwe mara moja.
Gavana Shilatu aliyasema hayo katika Kijiji cha Miuta kilichopo Kata ya Miuta, Tarafa ya Mihambwe mara baada ya kuletewa malalamiko na Wananchi juu ya kichaka hicho na kwenda kujiridhisha ambapo aliwaagiza Watendaji washirikiane na Wananchi kuhakikisha wanaondoa kichaka hicho mara moja ili kujiepusha na viumbe hatarishi kama Nyoka na Kenge.
"Ni Jambo la aibu suala la usafi mpaka Afisa Tarafa atoe maagizo wakati ni jukumu la kila mmoja kwa usalama wa afya na uhai wetu. Nawaagiza Watendaji mshirikiane na Wananchi kuhakikisha mnafyeka kichaka hiki na kisitokee kikaota tena. Nitafuatilia utekelezaji wake," alisema Gavana Shilatu.
Gavana Shilatu amesisitiza suala la usafi ni la kila Mtu kwa usalama wa afya na uhai wetu. Katika ziara hiyo ya kutembelea eneo hilo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Miuta, Watendaji Vijiji pamoja na Wananchi ambao walionyesha furaha kwa kero yao kusikilizwa na kutatuliwa kwa haraka.
No comments:
Post a Comment