Prof Idissa Rai |
Na Abdi
Shamna, Ikulu Zanzibar
MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof Idissa Rai amesema mahafali ya mwaka huu yameandika historia mpya kwa Chuo
hicho kutowa wahitimu wa fani ya Udaktari hapa nchini. Prof. Rai amesema hayo katika hafla ya
Mahafali ya 14 ya SUZA yaliofanyika katika viunga vya Chuo hicho Tunguu, Mkoa
wa Kusini Unguja.
Alisema uanzishaji wa masomo
hayo ni utekelezaji wa agizo la Rais
alilolitowa katika mahafali ya mwaka 2011, kwa lengo la kuhakikisha Zanzibar
inajitegeme kwa wataalamu wa fani nhiyo. Alisema hatua ya Chuo hicho kutowa
wahitimu 25 wa fani hiyo inatowa muelekeo mzuri wa kufikia malengo hayo.
Aidha, alitumia fursa hiyo
kuwapongeza Dk. Mohamed Jidawi na Dk. Jamala kwa mchango mkubwa iliofanikisha
kuanzishwa kwa fani hiyo chuoni nhapo. Pro. Rai, aliipongeza Serikali ya
watu wa Cuba kwa mashirkiano na mchango mkubwa uliowezesha kufanyika kwa
mafunzo hayo.
Alisema baada ya Serikali kufikia
uamuzi wa kukiimarisha chuo hicho na kukiunganisha na taasisi mbali mbali, chuo
kilichukuwa hatua za kuanzisha masomo katika fani mpya pamoja na kuweka
vipaumbele na mikakati madhubuti.
Alisema mambo muhimu yaliozingatiwa
kufanikisha malengo hayo ni pamoja na kujenga uwezo kwa wanataaluma , kujenga
miundombinu mipya na kukarabati ile iliopo ili iendane na fani husika. Alisema hivi sasa chuo kimo katika
maandalizi ya kuanzisha fani ya Udaktari wa meno, sambamba na malengo ya baadae
ya kuanzisha masomo ya Ubaharia.
Aidha, alisema Progaramu ay kazi ya
mafunzo ya Utalii, ina lengo la kutoa taswira nzuri ya shughuli za utalii ili kupanuwa wigo wa ajira kwa
vijana wa Kizanzibari kupitia sekta hiyo. Aliupongeza uongozi na wahadhiri wa
chuo hicho kwa kazi kubwa wanayofanya kwa maendeleo ya chuo hicho.
“Uongozi wa Chuo unathamini sana
juhudi zenu,tuongeze bidii katika kazi zetu na kuzidisha uzalendo kwa nchi
yetu, ili changamooto mbali mbali zinazotukabili zisiwe kikwazo katika kufikia
Dira na dhamira za chuo”, alisema Pro. Rai.
Nae, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu an
Mafunzo ya Amali Dk. Idrissa Muslih Hija, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza
hilo, alisema mahafali ya mwaka huu
imepanua wigo kwa kuongezeka fani mbili zaidi, tofauti na mwaka uliopita.
Alizitaja fani zilizoongezeka ni pamoja na Shahada ya Udaktari (doctor of
Medicine) pamoja na Cheti cha uanagenzi (certificate of Apprentenship katika masuala ya Utalii.
Alisema hatua hiyo imetowa matumaini
ya kuongezeka kwa idadi ya madaktari katika Hospitali hapa nchini, na
kuondokana an tatizo la uhaba wa madaktari uliopo.
Alisema fani hizo ni muhimu katika
kuimarisha maendeleo ya nchi na ustawi wa watu wake, kwani mafunzo waliyoyapata
yalizingatia mahitaji ya jamii.
Dk. Idrisa alitumia fursa hiyo
kuwapongeza washirika wa maendeleo kwa juhudi na mchango wao mkubwa katika
kukiendeleza Chuo hicho kupitia nyanja tofauti.
Alizitaja taasisi na mashirika hayo
kuwa ni pamoja na Milele Foundation. UNICEF,World Bank, NORAD, DANIDA, HUAWEI,
Ubalozi wa Uturuki, Serika ya Watu wa China
pamoja na Falme za Kiarabu.
Nae, Waziri wa Elimu na Mafgunzo ya
Amali, Riziki Pembe Juma aliipongeza serikali kw ajuhudi kubwa inazoendelea
kuchukuwa kuiendeleza sekta ya elimu nchini, ikiwemo ya elimu ya juu.
Alisema hatua ya Serikali kuongeza bajeti ya
upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka shilingi Bilioni 6.8 hadi Bilioni
11 imetowa fursa ya kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata mikopo hiyo
No comments:
Post a Comment