KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc, leo imezindua kampeni
kabambe ya data iitwayo “Data Datani’ ambayo inawezesha wateja wake kupata bonus
Mb hadi mara mbili zaidi kila wanunuapo bando la intaneti. Kampeni hiyo imezinduliwa
katika viwanja vya Mbagala Zackhem jijini Dar es Salaam.
Kampeni ya Data datani inalenga kuwawezesha watumiaji wa intanet kufaidi
zaidi matumizi ya vifurushi vyao na pia kuwajuza mbinu mbali mbali za kutunza
data isiishe kwa haraka, jambo ambalo limekuwa likiwatatiza wateja wake kwa
muda mrefu.
Ili kupata ofa hii, wateja wa Vodacom Tanzania Plc wanatakiwa kupiga
*149*01# kisha chagua intaneti, halafu chagua intaneti bando kisha nunua
kifurushi, hii itakuwezesha kupata hadi mara mbili ya bando uliyonunua awali
kwa bei ile ile.
Katika Uzinduzi wa kampeni hiyo kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom
Tanzania Plc, Linda Riwa alitilia mkazo umuhimu wa data katika maisha ya kila
siku. “Tukiwa ni Kampuni inayoongoza nchini kwa kutoa intaneti yenye kasi zaidi
nchini, ni muhimu kuzingatia pande zote mbili za sarafu, yaani huduma na wateja
wetu.
Ndio maana tumeleta kampeni hii ili kuwawezesha wateja wetu kupata zaidi
ya kile walicholipia kila wanaponunua bando la data,” alisema Linda huku
akiongeza kwamba wanafahamu umuhimu wa data hasa katika zama hizi za
kidijitali, habari zote na biashara ziko mitandaoni, hivyo wasingependa ukosefu
wa data uwe kikwazo kwa wateja wao katika kufanikisha shughuli zao za kila
siku.
Mwaka 2017 Kampuni ya Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa 4G katika
mkoa wa Dar es Salaam ili kuwawezesha wateja wake kupata intaneti yenye kasi
zaidi, na mpaka sasa mtandao huu wa 4G umesambaa kufikia mikoa 24.
Mmoja wa wafanyabiashara na mkaazi wa Mbagala aliyehudhuria uzinduzi huu
naye alisema, “Sasa ni wakati wa kudata datani, internet sio tu teknolojia bali
pia ni kiuwezeshaji. Inatuwezesha kupata habari haraka, inatuwezesha kufanya
biashara za mtandaoni, inawezesha serikali kupata kipato na kuwezesha shughuli
za kijamii, yani kudata, ni zaidi ya data tu”.
Kampeni hii inalenga kuwezesha wateja kutumia data zaidi na kikamilifu
kwa shughuli zao zote za mtandaoni bila kuwa na wasiwasi wa data kuisha.
Ili mteja aweze kufurahia huduma hii anapaswa kununua kifurushi kupitia
mfumo wowote iwe ni M-Pesa, vocha, My Voda App, na ataweza kuperuzi habari,
kuangalia video, kusikiliza muziki au kununua bidhaa mtandaoni. Changamkia
fursa hii kwa kubofya *149*01, pata kifurushi chako cha intaneti uendelee
kudata datani.
ABOUT
VODACOM
Vodacom
Tanzania PLC is the leading mobile communication service provider with the
fastest data network in the country. We provide communication services to over
14 million subscribers. Vodacom Tanzania and its subsidiary companies are part
of the Vodacom Group registered in South Africa which is in turn owned by
Vodacom Group Plc of the United Kingdom.
It has been registered in the Dar es
Salaam Stock Exchange (DSE) with registration number ISIN: TZ1886102715 Stock
name: VODA. For further information please visit our website: www.vodacom.co.tz
No comments:
Post a Comment