YANGA NA NAMUNGO, UWANJA WA MAJALIWA RUANGWA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 21 March 2019

YANGA NA NAMUNGO, UWANJA WA MAJALIWA RUANGWA...!

Andrew Vincent wa Yanga akizuia mpira kwa kichwa huku akizongwa na  Reliant Lusajo wa Namungo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwa Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1 – 1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mashabiki wa Yanga wakishangilia wakati timu yao ilipofunga bao katika mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo  na Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018.  Timu hizo zilitoka sare 1-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Deus Kaseke wa Yanga akimili mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Namungo iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare  1 – 1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu baada ya kukagua timu za Yanga na Namungo zilizocheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kulia kwake ni mkewe Mary , wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Timu hizo zilitoka sare 1-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment