WANAFUNZI WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA VODACOM TANZANIA KUPATA MAFUNZO YA UFANYAJI KAZI KIDIGITALI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 16 March 2019

WANAFUNZI WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA VODACOM TANZANIA KUPATA MAFUNZO YA UFANYAJI KAZI KIDIGITALI

Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Christina Murimi, akigawa vifaa kwa wanafunzi waliotembelea ofisi za Vodacom kujifunza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo. Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake dunianiVodacom iliwakaribisha wanafunzi hao wa kike kutoka shule  mbalimbali na  kuwapatia mafunzo ya ufanyaji kazi wa  kidijitali katika idara na vitengo vya kampuni hiyo.

Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Chambua akizungumza juu ya umuhimu wa elimu kwa  wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za kanda ya kati walipotembelea ofisi za kampuni ya Vodacom jijini Dodoma. Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao na  kuwapatia mafunzo juu ya ufanyaji kazi wa idara na vitengo mbalimbali katika sekta ya mawasiliano.

Mtendaji Mkuu wa  kampuni ya VodaCom Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Macfydene Minja (kushoto)  akionesha bango lenye orodha ya viwango vya kutoa pesa vinavyotozwa wakati wa kutoa fedha kwenye Mpesa kwa wanafunzi wa Sekondari kutoka mikoa saba ya kanda hiyo ambao wamechaguliwa katika mradi wa Interantional Girls in ICT kwa ajili ya kushindani katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Wasichana ya TEHAMA, walipofika katika makao makuu ya Vodacom kanda hiyo zilizopo Uhindini Jijini Mbeya ili kujifunza.

No comments:

Post a Comment