Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ikiwa ni maadhimisho ya Siku Haki ya Walaji ambayo hufanyika kila Machi 15 ya kila Mwaka.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwasikiliza TCRA Kanda ya Mashariki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani ambayo hufanyika Machi 15 ya Kila Mwaka.
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Joyce Paul akitoa maelezo kuhusiana utendaji wa mamlaka katika udhibiti wa mawasiliano wakati Kanda ya Mashariki TCRA ilipokwenda kutoa elimu katkka shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TCRA Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyofatilia mawasiliano wakati akitoa elimu katika Shule ya Sekondari Minaki ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Joyce Paul akitoa maelezo kuhusiana utendaji wa mamlaka katika udhibiti wa mawasiliano wakati Kanda ya Mashariki TCRA ilipokwenda kutoa elimu katkka shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TCRA Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyofatilia mawasiliano wakati akitoa elimu katika Shule ya Sekondari Minaki ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.
Na Josephat Lukaza
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imeendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa Umma kuhusiana na Maswala mbalimbali yanayohusu mitandao na mawasiliano kwa ujumla kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Minaki iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Mapema Jana Machi 15, 2019 ambao imeadhimisha siku ya Haki ya Watumiaji wa Huduma Mbalimbali inayoadhimishwa kila tarehe 15 Machi ya kila mwaka.
Zoezi hilo likiongozwa na Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Bw. Lawi Odielo pamoja na maafisa wengine kutoka Mamlaka hio wamefanikiwa kutoa elimu mbalimbali kuhusiana na matumizi sahihi ya mitandao ya Kijamii, Matumizi sahihi ya Simu za Mkononi pamoja na vifaa vya mawasiliano huku wakitoa elimu kuhusiana na Sheria za Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya EPOCA.
Katika Zoezi hilo lililofanyika Katika Shule ya Sekondari ya Minaki iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoa Pwani wanafunzi walifanikiwa kuelimishwa juu ya namna mbalimbali ya kujilinda na utapeli unaofanyika kupitia kwenye simu za mkononi kama vile "Ile Pesa Tuma Kwenye Namba Hii" kwa kuwaelekeza kabla ya kutuma pesa ni vyema wakahakiki kwa kumpigia simu kabla ya kutuma hata kama ujumbe huo utakuwa umetumwa na mtu anayemfahamu. Pia wameeleza kuwa Kwa kiasi kikubwa Mamlaka imeweza kupambana na matepeli hao na kuwachukulia sheria wale wote wanaovunja sheria kupitia Mitandao kwa Kusambaza habari za Uongo, picha za ngono, utapeli wa kutumia simu.
Wanafunzi pia walipata nafasi ya kuuliza maswali na kupewa majibu huku zoezi la kuwapa zawadi wanafunzi hao ambao pia waliweza kuulizwa maswali mbalimbali na waliopatia basi waliweza kukabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo Flash, Vikombe na Mifuko yenye nembo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Akiongea na Wanafunzi hao Mkuu wa kanda ya Mashariki Bw. Lawi Odielo alisema kuwa Wanafunzi wanapaswa kutumia mitandao kwa faida tena katika kutafuta masomo mbalimbali ya kujifunza kupitia mtandao na kuacha kupoteza muda wao kwa kutumia mitandao kwa vitu visivyo vya maana.
Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki wanaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa Umma kwaajili ya kuhamasisha watumiaji wa mitandao na huduma za mawasiliano kutumia vizuri na kuweza kufuata taratibu pindi wateja wa mawasiliano wanapokuwa hawajaridhika kutoka na huduma kuliko kubaki na kunung'unika tu.
No comments:
Post a Comment