SERIKALI YAPATA MKOPO WA MASHARTI NAFUU BILIONI 589.26 TOKA AfDB, KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA YA KAKONKO–KASULU-MANYOVU KM 260 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 6 March 2019

SERIKALI YAPATA MKOPO WA MASHARTI NAFUU BILIONI 589.26 TOKA AfDB, KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA YA KAKONKO–KASULU-MANYOVU KM 260

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni 589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya  mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akionesha mkataba wa mkopo wa masharti nafuu pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment