MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAZISHI YA MTOTO WA WAZIRI KIGWANGALLA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 22 February 2019

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAZISHI YA MTOTO WA WAZIRI KIGWANGALLA

Mazishi ya  mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla yakifanyika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla kwenye mazishi ya  Zulqarinain mtoto wa Waziri Dkt.Kigwangalla.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan  ameongoza  shughuli za  mazishi  ya  Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla  yaliyofanyika  Februari 22, 2019 saa kumi jioni katika kijiji cha Puge,  Nzega vijijini jimboni kwa Waziri Kigwangalla.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na   viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri Wabunge pamoja  na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Marehemu Zul alifikwa na mauti  katika JAK
 AYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE  hospitali ya taifa ya Muhimbili  alikokuwa   amelazwa   akiwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

No comments:

Post a Comment